Pata taarifa kuu
SOKA-LIGI KUU YA UINGEREZA

Arsenal yaongoza katika ligi ya Uingereza

Klabu ya Arsenal wanaongozakatika ligi ya Uingereza kwa pointi 39 baada ya kuiburuza Bournemouth kwa mabao 2-0.

Kikosi cha klabu ya Arsenal.
Kikosi cha klabu ya Arsenal. REUTERS/Eddie Keogh
Matangazo ya kibiashara

Arsenal wamepata ushindi huo kupita kwa wachezaji wake nyota wawili, ikiwa ni pamoja na Gabriel Paulista aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 27 ya mchezo, na katika dakika 63 ya mchezo Mesut Ozil, kiungo wa Kijeruman aliingiza bao la pili, na hivyo hadi kipenga cha mwisho, Bournemouth ilijikuta imeangukia pua kwa kufungwa mabao 2-0.

Wakati huo huo Manchester United wametoka sare ya kutofungana na mabingwa watetezi Chelsea.

Crystal Palace imetoka sare ya 0-0 na Swansea, huku Norwich ikiibwagiza Aston Villa mabao 2-0. Watford imefungwa na Tottenham 1-2, Newcastle imeifunga West Brom 1-0, huku West Ham ikiimenya Southampton 2-1.

Kwa upande mwengine Everton wakicheza katika uwanja wao wa Goodson Park wamefungwa kwa mabao 4-3 dhidi ya Stoke city.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.