Pata taarifa kuu
DRC-VITA CLUB-SOKA

DRC: As Vita Club yatupwa nje ya michuano

Klabu ya Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeondolewa nje ya michuano ya Shirikisho barani Afrika licha ya kupata ushindi wa mabao 3 kwa 2 dhidi ya Stade Malien katika mechi ya mwondoano mwishoni mwa juma lililopita.

Uwanja wa Kimataifa wa Tata Raphael jijini Kinshasa,ambapo imepigwa mechi ya As Vita Club na Stade Malien kutoka Mali..
Uwanja wa Kimataifa wa Tata Raphael jijini Kinshasa,ambapo imepigwa mechi ya As Vita Club na Stade Malien kutoka Mali.. capture d'écran youtube
Matangazo ya kibiashara

Mchuano huo ulichezwa katika uwanja wa Kimataifa wa Tata Raphael jijini Kinshasa.

Stade Malien ilifuzu baada ya kupata ushindi katika mchuano wa mzunguko wa kwanza kwa kuwashinda AS Vita Club mabao 2 kwa 0 jijini Bamako.

Vita club walistahili kupata ushindi wa mabao 3 bila ya kufungwa, kuwa na uhakika wa kusonga mbele, lakini vijana wa kocha Florent Ibengé walishindwa kulifanikisha hilo.

Msimu uliopita, AS Vita Club ilifika katika hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Afrika.

Katika matokeo mengine, Orlando Pirates ya Afrika Kusini imefuzu kwa jumla ya mabao 6 kwa 1 baada ya kuishinda Kaloum Star ya Guinea.

Etoile du Sahel ya Tunisia licha ya kupoteza mchuano wa kwanza dhidi ya Raja Casablanca ya Morroco.

CS Sfaxien ya Tunisia pia imefuzu baada ya kuishinda ASEC ya Cote Dvoire.

Sanga Balende ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikaoondolewa na Zamalek ya Misri.

Vlabu vingine vilivyofuzu katika hatua ya robo fainali ni pamoja na ES Tunis ya Tunisia, Al Ahly ya Misri na AC Leopard ya Congo Brazaville.

Michuano ya robo fainali nyumbani ya ugenini zimeratibiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu, na Esperance de Tunis, Etoile du Sahel zote za Tunisia, Al-Ahly ya Misri na Stade Malien ya Mali zimejumuishwa katika kundi moja.

Kundi lingine ni pamoja na Zamalek ya Misri, CS Sfaxien ya Tunisia, AC Leopards ya Congo na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.