Pata taarifa kuu
DRC-SOKA

DRC: Lushoises OCL City mabingwa wa soka taji la wanawake

Lushoises OCL City ndio mabingwa wa soka taji la wanawake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuwashinda Recoilless ya Mbuji-Mayi mabao 3 kwa 0 katika mechi ya fainali.

Uwanja wa mpira wa miguu Tata Raphaël wa mjini Kinshasa.
Uwanja wa mpira wa miguu Tata Raphaël wa mjini Kinshasa. capture d'écran youtube
Matangazo ya kibiashara

Hili ni taji la nne mfululizo kwa klabu ya Lushoises, iliyoanza kushiriki soka la wanawake nchini humo tangu mwaka 2012.

Mwaka uliopita, vilabu hivi vilikutana tena katika hatua ya fainali na akina dada kutoka Lubumbashi wakaendelea kudhihirisha kuwa wao ni moto wa kuotea mbali.

Nafasi ya tatu ilinyakuliwa na Bafana Bafana Katanga baada ya kuwafunga Mornng Star kutoka North Kivu mabao 6 kwa 1.

Mikoa 9 kati ya 11 ilishiriki katika makala haya ya nane ya michuano hii huku mikoa ya Kasai Occidental na Ecuador ikijiondoa kwa sababu za changamoto za kifedha.

Orodha ya vlabu vilivyoshiriki katika ligi hiyo:

Bilenge (Kinshasa)
Bafana Bafana (Katanga)
RC Boa (Maniema)
Promo Sport (Bas-Congo)
GTT (Bandundu)
Attack recoilless (Kasai Oriental)
Morning Star (South Kivu)
OCL into City (Katanga)

Orodha ya mabingwa wa taji hilo

Mwaka 2008 South Kivu
Mwaka 2009 Kinshasa
Mwaka 2010 Kinshasa
Mwaka 2011 Katanga
Mwaka 2012 OCL City
Mwaka 2013 OCL City
Mwaka 2014 OCL City
Mwaka 2015 OCL City.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.