Fifa yawachukulia hatua viongozi 2 wa Fecofoot
Viongozi wawili wa Shirikisho la soka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefungiwa kwa muda kushiriki katika shughuli za soka kwa kukeuka kanuni za Shirikisho la soka duniani Fifa.
Imechapishwa:
Makamu wa rais wa Fecofoot Jean Guy Blaise Mayolas na Katibu Mkuu Badji Mombo Wantete hawaruhusiwi kushiriki katika maswala ya soka kitaifa na kimataifa.
FIFA inasema hatua hiyo imechukuliwa baada ya Ofisi ya uchunguzi ikiongozwa na Cornel Borbély, akitumia kanuni ya sheria za FIFA kifungo 83 sehemu ya 1.
Haijaelezwa ni kwanini viongozi hao wawili wamepigwa marufuku kushiriki katika maswala ya soka.
Wakati huo huo Shirikisho la soka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Fecofoot, limetangaza rasmi ratiba ya kuwania ubingwa wa taji la msimu huu la taifa “Congo cup” kuanzia juma lijalo.
Michuano 72 itachezwa katika miji ya Kinshasa, Lubumbashi na Bukavu.
Michuano ya kwanza itachezwa kuanzia tarehe 8 jijini Kinshasa, huku vilabu kutoka Kivu Kusini vikimenyana kuanzia tarehe 16.
Kutakuwa na makundi mawili katika michuani hii na watakaomaliza wa kwanza katika kila kundi watacheza mechi ya fainali mjini Lubumbashi.
Hii ndio ratiba kamili ya michuano hiyo :
Mjini Kinshasa
Kundi A / uwanja wa Tata Raphaël
Juni 8 mwaka 2015: AS Veti Club vs DCMP / Bumba , Renaissance FC vs AS Vutuka
Juni 10 mwaka 2015: DCMP / Bumba vs FC Renaissance , AS Vutuka Veti vs Club
Juni 15 mwaka 2015: AS Vutuka vs DCMP / Bumba , AS Veti vs FC Club Renaissance
Kundi B / uwanja wa Tata Raphaël
Juni 9 mwaka 2015: FC MK vs Shark XI FC
Juni 11 mwaka 2015: Shark XI FC vs DC Motema Pembe
Juni 16 mwaka 2015: DC Motema Pembe vs MK
Uwanja wa Bukavu
Kundi A /uwanja wa Concorde
Juni 10 mwaka 2015: Ndjadi vs. El Dorado , OC Bukavu Dawa Nyuki vs AS Vita
Juni 12 mwaka 2015: El Dorado vs OC Bukavu Dawa , Ndjadi Nyuki vs AS Vita
Juni 14 mwaka 2015: AS Nyuki vs El Dorado , vs OC Bukavu Dawa Ndjadi
Kundi B /Uwanja Concorde
Juni 11 mwaka 2015: AS Nika vs AS Capaco , AS Black Dolphins vs AS Makiso
Juni 13 mwaka 2015: Black Dolphins vs AS Capaco , AS Nika vs AS Makiso
Juni 15 mwaka 2015: AS Black Dolphins vs AS Nika (1:45 p.m.), AS Makiso vs Capaco
Mjini Lubumbashi
Kundi A / Uwanja wa TP Mazembe
Juni 10, mwaka 2015: KFA vs AS Saint Luke
Juni 12 mwaka 2015: US Kasai vs AS Saint Luc
Juni 14 mwaka 2015: US KFA vs Kasai
Kundi B / Uwanja wa Kibasa Maliba
Juni 9 mwaka 2015: US Lubumbashi Sport vs Tshinkunku , AS Bantu vs FC St. Eloi Lupopo , JS Group Bazano vs SM Sanga Balende
Juni 11 mwaka 2015: AS Bantu vs JS Bazano Group, Lubumbashi FC Sport vs SM Sanga Balende , US vs FC Saint Eloi Tshinkunku Lupopo , US Tshinkunku vs FC Saint Eloi Lupopo
Juni 13 mwaka 2015: AS Bantu vs FC Sport Lubumbashi , SM Sanga Balende vs US Tshinkunku , JS Group Bazano vs FC St. Eloi Lupopo
Juni 15 mwaka 2015: US Tshinkunku Bazano vs JS Group , AS Bantu vs SM Sanga Balende , FC Saint Eloi Lupopo vs Lubumbashi Sport
Juni 17 mwaka 2015: US Tshinkunku vs AS Bantu , JS Group Bazano Lubumbashi Sport vs FC , SM Sanga Balende vs FC St. Eloi Lupopo