Pata taarifa kuu

Israel yatangaza kuwahamisha takriban watu 100,000 kutoka mashariki mwa Rafah

Jeshi la Israel limeanza shughuli ya kuwahamisha "takriban watu 100,000" wanaoishi mashariki mwa Rafah leo Jumatatu, na kuwataka kuhamia "maeneo yaliyotengwa watu salama". 

Wapalestina wakikagua vifusi baada ya mashambulizi ya Israel huko Rafah, Mei 6, 2024.
Wapalestina wakikagua vifusi baada ya mashambulizi ya Israel huko Rafah, Mei 6, 2024. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya hayo, juhudi za kufikia makubaliano ya usitishwaji vita katika Ukanda wa Gaza kati ya Israel na Hamas zimeshindwa kuduati misimo ya kambi zote mbili, mkwamo ambao wapatanishi wa kimataifa watajaribu kuutatua siku ya Jumatatu wakati wa "mkutano wa dharura" nchini Qatar

Licha ya onyo la kimataifa, Benjamin Netanyahu bado anatishia kuanzisha operesheni ya kijeshi huko Rafah.

Serikali ya Israel "imeamua kwa kauli moja" kwamba kituo cha habari cha Al-Jazeera "kitafungwa nchini Israel", ametangaza Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Wakati huo huo Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu, OIC, imelaani kile imekitaja kuwa "mauaji ya halaiki" kwenye Ukanda wa Gaza.

OIC Pia imetoa mwito kwa nchi wanachama kuiwekea vikwazo Israel na kusitisha mara moja kuiuzia silaha nchi hiyo.

Katika tamko la mwisho la mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo uliofanyika nchini Gambia, OIC, imeyarai mataifa 57 wanachama kutumia shinikizo la kidiplomasia, kisiasa na kisheria na kuchukua hatua zozote zitakazosaidia kumaliza kile imekiita "vita vya Israel dhidi ya umma wa Wapalestina."

Pia imetoa mwito wa kupatikana makubaliano ya haraka na ya kudumu ya kusitishwa mapigano.

OIC ambayo iliundwa mwaka 1969 kufuatia kuchomwa moto kwa msikiti wa al-Aqsa, ambao ni moja ya maeneo tukufu kwa waislamu, ina malengo ya kupigania mshikamano miongoni mwa waislamu, kuunga mkono harakati za uhuru wa Palestina na kuyalinda maeneo muhimu ya dini ya kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.