Pata taarifa kuu

Afghanistan: Takriban watu 16 wauawa katika mlipuko dhidi ya shule ya Quran

Takriban watu 16 wameangamia katika mlipuko dhidi ya shule ya Quran kaskazini mwa Afghanistan, chanzo cha hospitali kimesema leo Jumatano.

Makumi ya milipuko na mashambulizi yaliyolenga raia yametokea tangu Taliban iliporejea madarakani Agosti 2021, mashambulizi ambayo mengi yakidaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (I-K) la eneo hilo.
Makumi ya milipuko na mashambulizi yaliyolenga raia yametokea tangu Taliban iliporejea madarakani Agosti 2021, mashambulizi ambayo mengi yakidaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (I-K) la eneo hilo. AP - Ebrahim Noroozi
Matangazo ya kibiashara

 

"Takriban watu 16 wameuawa na 24 kujeruhiwa Jumatano, Novemba 30, katika mlipuko uliotokea katika shule ya Quran katika mji wa Aybak, kaskazini mwa Afghanistan, " kulingana na chanzo cha hospitali.

Mlipuko ulitokea katika mji wa Aybak, Kaskazini mwa Afghanidtan.

"Wote ni watoto na watu wa kawaida," daktari katika hospitali ya Aybak, mji mkuu wa mkoa wa Samangan, yapata kilomita 300 kaskazini mwa Kabul, ameliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina.

Afisa wa mkoa huo amethibitisha mlipuko huo, lakini hakuweza kutoa takwimu za majeruhi au habari kuhusu hali hiyo. "Wachunguzi wetu na vikosi vya usalama vinafanya kazi haraka kubaini waliohusika na uhalifu huu usiosameheka na kuwaadhibu kwa vitendo vyao," ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Abdul Nafay Takor, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani.

Tawi la ndani la IS lanyooshewa kidole

Makumi ya milipuko na mashambulizi yaliyolenga raia yametokea tangu Taliban iliporejea madarakani Agosti 2021, mashambulizi ambayo mengi yakidaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (I-K) la eneo hilo.

Shambulio la kujitoa mhanga mnamo Septemba 30 katika kituo cha mafunzo cha Kabul kinachojiandaa kwa mitihani ya chuo kikuu kiliua watu 54, wakiwemo wasichana wasiopungua 51, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Shambulio hili halikudaiwa na kundi lolote, lakini serikali ya Afghanistan ilishutumu kundi la I-K kwa kutekeleza shambulio hili.

Tarehe 5 Oktoba, watu wasiopungua wanne waliuawa mjini Kabul katika mlipuko uliotokea katika msikiti wa Wizara ya Mambo ya Ndani.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.