Pata taarifa kuu

Kundi la IS lamteua kiongozi mpya, lathibitisha kifo cha Abu Ibrahim al-Qurachi

Kundi la wanajihadi la Islamic State (IS) limethibitisha kifo cha kiongozi wake Abu Ibrahim al-Qurachi na kumtaja mrithi wake Abu Hassan al-Hashemi al-Qurachi, kulingana na taarifa iliyotolewa Alhamisi wiki hii.

Vikosi vya Iraq vikiendesha mashambulizi dhidi ya ngome ya kundi la IS,  Falluja, Mei 30, 2016 .
Vikosi vya Iraq vikiendesha mashambulizi dhidi ya ngome ya kundi la IS, Falluja, Mei 30, 2016 . REUTERS/Alaa Al-Marjani
Matangazo ya kibiashara

Wanajihadi wa IS "wamekula kiapo cha utii kwa Abu Hassan al-Hashemi al-Qurachi, amiri wa waumini na khalifa wa Waislamu", msemaji wa kundi hilo amesema katika sauti iliyorekodiwa, wakati akithibitisha kifo cha kiongozi wa zamani wa IS na msemaji wake wa zamani.

Kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa IS pamoja na msemaji wake wa awali pia vimethibitishwa katika sauti iliyorekodiwa.

"Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurachi na msemaji rasmi wa Dola ya Kiislamu (...) Abu Hamza al-Qurachi waliuawa hivi karibuni," ameongeza msemaji huyo mpya.

Kiongozi wa zamani wa IS alijilipua wakati wa operesheni ya kikosi maalum cha Marekani kaskazini magharibi mwa Syria, eneo lililo chini ya udhibiti wa wanajihadi, Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza Februari 3. mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.