Pata taarifa kuu

Marekani yamuua kiongozi wa IS nchini Syria

Kiongozi wa kundi la Islamic State (IS), Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurayshi, aliuawa wakati wa operesheni iliyofanywa kaskazini mwa Syria, ametangaza Rais wa Marekani Joe Biden Alhamisi hii Februari 3. Wanajeshi wote wa Marekani wako salama salimini, amesema.

Rais wa Marekani Joe Biden, Februari 3, 2022.
Rais wa Marekani Joe Biden, Februari 3, 2022. AFP - SAUL LOEB
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi, Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa kiongozi wa kundi la Islamic State aliuawa katika operesheni ya jeshi la Marekani nchini Syria usiku wa Jumatano Februari 2 kuamkia Alhamisi Februari 3.

Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurayshi aliuawa katika mlipuko aliojisababishia mwenyewe. "Mwanzoni mwa operesheni hiyo, mlengwa wa kigaidi alilipua bomu ambalo lilimuua yeye na watu wa familia yake, wakiwemo wanawake na watoto," afisa mkuu wa Ikulu ya White House amesema.

Vikosi maalum vya Marekani vilisafirishwa kwa helikopta kabla ya alfajiri siku ya Alhamisi katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Syria, operesheni ambayo ni nadra ya aina yake ambayo ilisababisha vifo vya watu 13, wakiwemo wanawake na watoto, kulingana na shirika moja lisilo la kiserikali.

Mnamo mwezi Oktoba 2019, shambulio kama hilo lilimwangamiza Abu Bakr al-Baghdadi, kiongozi wa zamani wa kundi la Islamic State.

 

Joe Biden ametangaza kuwa atahutubia wananchi wa Marekani baadaye Alhamisi hii asubuhi, saa za Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.