Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI-TALIBAN-USALAMA

Mazungumzo kati ya pande hasimu Afghanistan kuanza Doha

Serikali ya Afghanistan na kundi la Taliban wanaanza mazungumzo ya kihistoria ya amani huko Doha, nchini Qatar, leo Jumamosi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo anahudhuria mazungumzo hayo ambayo yanadaiwa kuwa magumu kwa sababu ya tofauti kubwa kati ya pande hizo mbili hasimu.

Wafungwa wa Taliban waachiliwa huru kulingana na makubaliano ya Loya Jirga, Agosti 9.
Wafungwa wa Taliban waachiliwa huru kulingana na makubaliano ya Loya Jirga, Agosti 9. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yamecheleweshwa kwa miezi sita kwa sababu ya kutokubaliana kwa kina juu ya ubadilishanaji wa wafungwa kati ya serikali na waasi.

Mazungumzo hayo yanafanyika siku moja baada ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 19 ya mashambulio ya Septemba 11, 2011, ambayo yalipelekea uingiliaji wa kimataifa ulioongozwa na Marekani, ambao uliwatimua Wataliban madarakani nchini Afghanistan.

Pande zote mbili zinatarajia kutafuta njia "ya kuindeleza mbele nchi hiyo ili kupunguza machafuko na kufikia mahitaji ya Waafghan.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani anatarajia kushiriki katika ufunguzi wa mazungumzo hayo na anatarajiwa baadaye Jumamosi huko Kupro.

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye atawania muhula wa pili katika uchaguzi wa urais wa Novemba 3, amedhamiria kumaliza vita vya kihistoria vya muda mrefu na Marekani.

Lakini suluhu ya haraka ya mzozo huo inaonekana kutiliwa mashaka na mazungumzo hayo haijulikani ni lini yatamalizika.

Taliban wametangaza kuwa wako tayari kushiriki mazungumzo hayo. "Kuna uwezekano mkubwa kwamba mazungumzo yataanza Jumamosi," chanzo cha Taliban kimethibitisha katika taarifa, na kusisitiza juu ya nia yao ya "kuendeleza mchakato wa mazungumzo" na "kuleta amani kamili na mfumo safi wa Kiislam ndani ya mfumo wa maadili yao ya Kiislamu na masilahi yao ya kitaifa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.