Pata taarifa kuu
CHINA-SAUDI ARABIA-USHIRIKIANO

Rais wa China Xi aanza ziara ya kikanda Saudi Arabia

Rais wa China Xi Jinping amewasili nchini Saudi Arabia Jumanne hii, ikiwa ni mwanzo wa ziara ya kikanda yenye lengo la kuimarisha uwepo wa kiuchumi kuanzia Asia hadi Mashariki ya Kati, shirika la habari la Saudi Arabia SPA limetangaza.

Rais wa China Xi Jinping amewasili Saudi Arabia kukuza ushirikiano wa kiuchumi na fedha kati ya mataifa hayo mawili.
Rais wa China Xi Jinping amewasili Saudi Arabia kukuza ushirikiano wa kiuchumi na fedha kati ya mataifa hayo mawili. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya kwanza ya kikanda ya Xi kama Rais wa China itampeleka Misri na Iran baada ya Saudi Arabia.

Riyadh na Tehran wako katika mvutano wa kidiplomasia tangu uatawala wa Saudi Arabia uchukuwe uamzi Januari 2 wa kumuua Mhubiri wa Kishia Nimr al-Nimr, kiongozi mkuu wa upinzani wa serikali ya Saudi Arabia aliyehukumiwa kwa kosa la "ugaidi."

Mauaji hayo yalisababisha mashambulizi dhidi ya balozi za Saudi Arabia nchini Iran, mashambulizi ambayo yamesababisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tehran na Riyadh yanavunjika.

Rais Xi anafika katika Ukanda wa Mashariki ya Kati baada ya kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi na kifedha dhidi ya Iran kutokana na utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia na mataifa yenye nguvu.

China ilikuwa ni moja ya nchi sita zenye nguvu duniani kwa kuweza kufanya mazungumzo kuhusu mkataba huu na Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.