Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Kenya: Mwanaume abomoa nyumba ya mashemeji wake kwa kuzuiwa kuoa binti wao:Uongo

Imechapishwa:

Kuna picha inayosambaa mitandaoni ikidai kuonyesha mwanaume akibomoa nyumba nchini Kenya baada ya mashemeji wake kukataa ombi la kumchumbia binti wao. Lakini huu ni uongo. Picha hii imekuwepo mtandaoni tangu Juni 2021.

Tukio hilo lilifanyika nchini Nigeria wakati polisi wakibomoa makazi ya washukiwa wa utekaji
Tukio hilo lilifanyika nchini Nigeria wakati polisi wakibomoa makazi ya washukiwa wa utekaji © FMM
Matangazo ya kibiashara

Chapisho la Julai 2 kwenye facebook, ilisoma hivi, “Mwanamume mwenye hasira katika Kaunti ya Bungoma nchini Kenya alibomoa nyumba aliyowajengea wazazi wa mpenzi wake baada ya kukataa ombi lake la ndoa,” Kaunti hii ya Bunguma iko magahribi mwa Kenya.

Msikilizaji picha na madai pia yalishirikiwa kwenye TikTok na hata kusambazwa facebook na twitter na makundi ya watsup.

Picha hizo hizo zilichapishwa katika chapisho Facebook mara hii zikidai zilionyesha nyumba iliyobomolewa hivi majuzi huko Sudan Kusini.

"Mwanamume mwenye hasira huko Gumbo Sherikat alibomoa nyumba ambayo aliwajengea wazazi wa mpenzi wake baada ya kukataa ombi lake la ndoa."

Madai haya ni ya uongo, utafiti kupitia reverse image search, Uchunguzi wa Ukweli wa AFP ambao pia tumeufanya,  uligundua kuwa picha hiyo imekuwa mtandaoni tangu Juni 2021.

Ni picha ambayo ilichapishwa na tovuti kadhaa za habari za Nigeria zilizoripoti juu ya ubomoaji huo katika jimbo la Benue, wakati serikali ya jimbo hilo ilitumia sheria ya kupinga utekaji nyara ili kuidhinisha ubomoaji huo.

Serikali ya Jimbo la Benue Jumatatu ilibomoa majengo mawili yanayodaiwa kuwa ya "jambazi na mtekaji nyara anayesakwa sana," alisema Cephas Shekere, almaarufu Azonto, katika maeneo tofauti huko Makurdi, mji mkuu wa jimbo hilo.

Taarifa za ubomozi huu na pia picha zilichapishwa na BBC kwenye kurasa zake za lugha ya mama nchini Nigeria. Wakati huu pia serikali ilisema ilichukua hatua hiyo ili iwe funzo ana onyo kwa wale wanaozuia amani katika jimbo hilo.

BBC ilitoa picha hizo kwa mwandishi wa habari anayeishi Nigeria Raphael Akume, ambaye alithibitisha kwa AFP Fact Check kwamba alipiga picha hizo.

Vipindi vingine
  • 10:18
  • 10:00
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.