Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

DRC: WFP na FAO zinapanga kuwapa M23 chakula: Sio Kweli

Imechapishwa:

Ujumbe ambao umekuwa ukisambaa nchini DRC unasema hivi, utata umepatikana kati ya utawala wa Rutshuru na kundi la M23, RDF, shirika la chakula na kilimo FAO na mpango wa WFP. Kutoka tarehe 10 Mei, mashirika haya yatakuwa yanatoa chakula kwa kundi la M23 na RDF.

Taarifa za kupotosha kwamba WFP na FAO zinawapa waasi wa M23 chakula
Taarifa za kupotosha kwamba WFP na FAO zinawapa waasi wa M23 chakula © FMM
Matangazo ya kibiashara

Ni taarifa ambayo iliendelea kusema kuwa mawakala watatoka nchini Rwanda na wataandikishwa na Pascal Rubumba and Sukaka Dieudonne.

Msikilizaji kwa muda mrefu sasa, mashirika yasiyo ya kiserikali kama vile WFP na mengine mengi, yamekuwa yakipakwa tope kupitia propaganda na habari za uongo nchini DRC.

Tumethibitisha na ofisi na WFP nchini DRC kupitia barua pepe, na huu ndio ujumbe waliotutumia:

Kwa sasa, WFP haiwezi kufanya mahojiano yoyote. Lakini mashirika ya WFP na FAO yanatoa hakikisho kwamba yataendelea kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia maadili, ili kuhudumia jamii zinazohtaji msaada wa kibinadamu, na hakuna hata wakati mmoja wataegemea upande mmoja au kutoa chakula kwa makundi ya kujihami.

Taarifa hiyo ilikuwa ya kupotosha tu raia

Vipindi vingine
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
  • 10:01
  • 10:16
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.