Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Taarifa za kupotosha kuhusu zaira ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron DRC

Imechapishwa:

Taarifa ya kupotosha inayotufungulia kipindi hiki cha UONGO au KWELI, ni kuhusu ziara ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliyoifanya nchini DRC mnamo Machi 4.Kwanza tuondoe dhana kuwa rais Macron aliwasili Kinshasa usiku kwa sababu ya hofu ya kuvamiwa ya raia, hii ni baada ya picha na video kuvuja mitandaoni zikionyesha raia wakiandamana katika ubalozi wa Ufaransa jijini Kinshasa

Rais wa Ufaransa Macron wakati wa ziara yake nchini DRC alisistiza kuwa Ufaransa inaunga mkono juhudi za kuleta amani katika eneo la mashariki.
Rais wa Ufaransa Macron wakati wa ziara yake nchini DRC alisistiza kuwa Ufaransa inaunga mkono juhudi za kuleta amani katika eneo la mashariki. © FMM-RFI
Matangazo ya kibiashara

Taarifa za kupotosha hazikwishi kwenye mitandao ya kijamii, ziara ya rais wa DRC Felix Tshisekedi huko Geneva ilipotoshwaje?

Mnamo Februari 27, wakuu wa nchi na mawaziri zaidi ya 100 walihudhuria kikao cha Baraza la UN kuhusu haki za binadamu mjini Geneva na rais Tshisekedi ni mmoja wa waliohudhuria.

Taarifa ya kupotosha ni kuhusu video iliyochapishwa chini ya nembo ya AFRIKAKOOL kwenye youtube ambapo Tshisekedi ametambulishwa katika mkutano huo kama waziri mkuu. Hii hapa hiyo video

Vipindi vingine
  • 10:18
  • 10:00
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.