Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Taarifa za uongo kuwa mshauri wa rais Tshisekedi alikamatwa na mkoba wa pesa

Imechapishwa:

Mfano kundi la Politic.net lilichapisha na kusema Mshauri wa Rais wa DRC, André_Tshibanda tshisabu, alikamatwa na idara ya Uhamiaji Kinshasa DGM, katika uwanja wa ndege wa N'djili akiwa na pesa taslimu zaidi ya dola elfu mia nane sza marekani, akitokea Brussels. Lakini mtandao huu baadaye uliondoa taarifa hii.

Kibonzo cha Dkt Meddy kikielezea taarifa feki kuwa mshauri wa rais wa DRC Felix Tshisekedi  AndréTshibanda tshisabu alikamatwa na mkoba wa pesa jijini Kinshasa
Kibonzo cha Dkt Meddy kikielezea taarifa feki kuwa mshauri wa rais wa DRC Felix Tshisekedi AndréTshibanda tshisabu alikamatwa na mkoba wa pesa jijini Kinshasa © FMM-RFI
Matangazo ya kibiashara

Naye Jérémie Masheki kwenye ukurasa wa facebook, aliandika ujumbe sawia na huo ukiwa na kichwa;  KUKAA MBELE YA MEZA ILIYO NA DOLA ZA MAREKANI KAMA NI DILI YA DHAHABU.

Lakini taarifa hizi hazikuwa za kweli. Kwenye mtandao wa twitter mnamo Februari 24, Ofisi ya rais Tshisekedi ilichapisha taarifa ikiwa na heshitegi Kinshasa ikisema Kitengo cha Mawasiliano cha Ofisi ya Rais, kinakanusha uvumi ulioenea kwenye mitandao ya kijamii ukiKwelidai kuwa mshauri Mkuu wa rais alikamatwa katika uwanja huo.

Vipindi vingine
  • 10:18
  • 10:00
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.