Pata taarifa kuu
UGANDA-ICC-ONGWEN-HAKI

Mahakama ya ICC yaanza kusikiliza tena kesi inayomuhusu Dominic Ongwen

Majaji kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya ICC, hivi leo wameanza kusikiliza maelezo ya mwisho kutoka kwa upande wa mashitaka na utetezi kwenye kesi inayomuhusu aliyekuwa kamanda msaidizi wa kundi la waasi wa Uganda la Lord Resistance Army (LRA), Dominic Ongwen.

Dominic Ongwen akisimama mbele ya majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC, Desemba 6, 2016.
Dominic Ongwen akisimama mbele ya majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC, Desemba 6, 2016. REUTERS/Peter Dejong/Pool
Matangazo ya kibiashara

Dominic Ongwen anakabiliwa na mashitaka kuhusu mauwaji, mateso, ubakaji na watu kugeuzwa watumwa, mashitaka ambayo anatakiwa ajieleze mbele ya mahakama hiyo ya kimataifa.

Dominic Ongwen na kundi lake la waasi la Lord's Resistance Army anatuhumiwa kuhusika na mauwaji ya watu zaidi ya laki moja tangu mwaka 1987 na kuwateka nyara maelfu ya watoto.

Anabidi ajibu mashitaka kuhusiana na uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinaadam katika kadhia 70 zilizotokea kati ya mwaka 2002 na 2005 kaskazini mwa Uganda.

Kesi yake ilifunguliwa kwa kuonyeshwa kanda za video na picha za miili ya watu iliyokatwa vipande vipande.

Mwendesha mashitaka mkuu Fatou Bensouda aliimtaja Ongwen kuwa " katili na mbakaji" na kwamba miongoni mwa wenye kuamrisha katika kundi hilo la waasi,"yeye ndie aliyekuwa habithi kuliko wote."

Visa vilivyotajwa hajakanusha kuwa vilitokea, lakini anadai vilifanywa na LRA na sio yeye. Na wakati kesi yake ilisikilizwa kwa mara ya kwanza aliapa kwa jina la Mungu akisema yeye hahusiki.

Usumbufu na mateso aliyo yapata alipotekwa nyara akiwa mdogo nayo pia hayasaidii kitu kwa kesi inayomkabili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.