Pata taarifa kuu
BURUNDI-HRW-SIASA-USALAMA

Vuguvugu la vijana kutoka chama tawala Burundi lashtumiwa katika visa vya unyanyasaji

Shirika la kimataifa la haki za Binadamu la Human Rights Watch limetoa ripoti kuhusu dhulma zinazohusiana na michango iinayotolewa na raia kwa hiari yao kwa minajili ya kufadhili uchaguzi wa mwaka 2020 nchini Burundi.

Kulingana na ripoti ya HRW , vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure,  walishiriki katika mauaji ya kikatili mkoani Cibitoke kati ya Desemba 30 na Januari 3.
Kulingana na ripoti ya HRW , vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure, walishiriki katika mauaji ya kikatili mkoani Cibitoke kati ya Desemba 30 na Januari 3. Desire Nimubona/IRIN/www.irinnews.org
Matangazo ya kibiashara

Serikali imekuwa ikiandaa kampeni ya kitaifa tangu mwishoni mwa mwaka 2017 ili kukusanya michango ya fedha za kutosha kuandaa uchaguzi huo. Lakini kulingana na ripoti ya Human Rights Watch, michango hii kwa kweli imekuwa ikichangishwa kwa nguvu na vuguvugu la vijana wa chama madarakani CNDD-FDD, Imbonerakure.

Human Rights Watch imesema ikinukuu mashahidi ilioweza kuongea nao, kwamba walilazimishwa kutoa michango hiyo mara kadhaa, wakati mwingine zaidi ya kiwango kilichotolewa na serikali. Kulingana na shirika hilo, kulikuwa na dhuluma nyingi kwa upande wa viongozi tawala katika maeneo mbalimbali ya nchi lakini pia vuguvugu la vijana wa chama tawala, Imbonerakure. Ripoti hiyo inabaini kwamba vuguvugu hilo la vijana wa chama tawala nchini Burundi linafanya kazi sambamba na polisi.

Vuguvugu ambalo halisiti kutumia vurugu na vitisho kulazimisha raia kutoa michango yao wakipenda wasipendi. Human Rights Watcha pia limebaini kwamba katika maeneo mengine, vijana hao wamekuwa wakiweka vizuizi barabarani kuwazuia watu ambao hawajatoa michango yao kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka wa 2020.

Shirika hilo linasema kuwa ili kupata huduma katika vituo vya afya au hospitalini, wagonjwa wamekuwa wakitakiwa kuonyesha risiti walizolipia kwa michango hiyo.

Human Rights Watch inahoji katika ripoti hiyo jukumu la Imbonerakure, ambayo haina mamlaka ya kisheria katika majukumu ya kiutawala kama vile kukusanya pesa.

Human Rights Watch ina wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa mvutano kabla ya Uchaguzi Mkuu Mei mwaka 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.