Pata taarifa kuu
KENYA-RUSHWA-UCHUMI-HAKI

Waziri wa Fedha wa Kenya akamatwa kwa madai ya rushwa

Waziri wa Fedha wa Kenya Henry Rotich na viongozi kadhaa wa wizara ya fedha wamekamatwa Jumatatu hii (Julai 22) kwa madai ya rushwa na udanganyifu kuhusiana na mradi wa ujenzi wa mabwawa mawili wenye thamani ya dola milioni mbili, polisi imetangaza.

Henry Rotich (kushoto) anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa mawili nchini.
Henry Rotich (kushoto) anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa mawili nchini. CS Henry K. Rotich/twitter.com
Matangazo ya kibiashara

"Watuhumiwa wanazuiliwa na wanasubiri kupelekwa mahakamani," mkuu wa polisi ya Kenya George Kinoti ameliambia shirika la Habari la AFP, akiongeza kuwa watuhumiwa hao wamejisalimisha kwa maafisa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya umma, Noordin Haji, kuomba hapo awali waweze kukamatwa.

"Henry Rotich anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa mawili nchini, " imesema taarifa kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Mashitaka ya umma.

Noordin Haji ameeleza kwamba watashtakiwa kwa "kupanga kufanya udanganyifu, kushindwa kutii muongozo unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi" miongoni mwa mambo mengine.

"Katiba yetu inasisitiza baadhi ya maadili yetu yakiwemo uadilifu… kuyatimiza hususan kwa walio uongozini, " ameongeza Mkurugenzi wa Mashitaka ya umma.

Maafisa wengine walioagizwa kukamatwa na kushtakiwa ni pamoja na katibu mkuu katika wizara ya fedha Kamau Thugge, Dkt Susan Jemutai Koech kutoka wizara ya jumuiya ya Afrika mashariki na mkurugenzi msimamizi wa mamlaka ya maendeleo ya Kerio Valley (KVDA) David Kimosop.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.