Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-MABALOZI-AMANI-FEDHA

Sudan Kusini kufunga Balozi zake 39 duniani kwa ukosefu wa fedha

Serikali ya Sudan Kusini imesema inapanga kufunga Balozi zake 39 nje ya nchi kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi.

Rais wa Sudan Kusini  Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje Mawien Makol, amesema Juba inapata shida kuendesha balozi hizo kwa sasa.

Aidha, ameongeza kuwa sababu ya kufunga balozi hizo ni kutumia fedha zitakazohifadhiwa ili kuendesha zile zinazosalia.

Uamuzi huu unaanza kutekelezwa haraka iwezekavyo.

Hatua hii imekuja, baada ya rais Salva Kiir wiki iliyopita kuwafuta kazi Mabalozi 40 ambao alisema walikuwa hawaendi kazini kwa muda mrefu.

Sudan Kusini ilipata uhuru mwaka 2011 na kutuma mabalozi katika mataifa mbalimbali lakini changamoto kubwa imekuwa ni kuanza kwa vita mwaka 2013.

Kumaliza mzozo wa Sudan Kusini kati ya rais Salva Kiir na Riek Machar, pande zote mbili zilitia saini mkataba wa amani, unataka kuundwa kwa serikali ya mpito, suala ambalo limeahirishwa hadi baadaye mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.