Pata taarifa kuu
KENYA-USALAMA

Askari watano wauawa kwa bomu la kutegwa ardhini Kenya

Askari watano wa Kenya wameuawa kwa mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini lililotengenezwa kienyeji wakati msafara wao ulikua ukielekea katika Kaunti ya Lamu, mashariki mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Somalia, jeshi limesema.

Askari wa Kenya wakipiga doria karibu na mpaka na Somalia
Askari wa Kenya wakipiga doria karibu na mpaka na Somalia RFI/Stéphanie Braquehais
Matangazo ya kibiashara

"Askari wanaohudumu katika Kaunti ya Lamu, ambao walikuwa katika ujumbe wa kibinadamu wa kutoa msaada wa maji kwa wakazi wa eneo hilo, wamshambuliwa kwa bomu la kutegwa ardhini," jeshi limesema katika taarifa yake, na kuongeza kuwa askari watano " wamepoteza maisha kufuatia majeruhi waliopata "huku wengine 10" wakiendelea kupata matibabu ".

Tukio hilo lilitokea kilomita chache kutoka mpaka wa Somalia, kati ya vijiji vya pwani ya Kiunga na Sankuri.

Matumizi ya mabomu yaliyotengenezwa kienyeji dhidi ya polisi na askari wanaopiga doria katika maeneo ya mpakani kaskazini na mashariki mwa Kenya, karibu na Somalia, ynatokea kila kukicha. Wanamgambo wa Kisomali wa Al-Shabab, kwa siku za nyuma wamekuwa wakidai kutekeleza mashambulizi kama haya ambayo yameua maafisa wengi wa usalama na askari wa Kenya.

Kundi la Al-Shabab lenye mafungamano na al-Qaeda, limeapa kuendelea na mashambulizi hadi kuhakikisha kuwa serikali ya Somalia inapoteza imani kwa wananchi.

Serikali ya Somalia inaendelea kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na askari 20,000 wa kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom), ambapo Kenya inashiriki wanaendelea kupambana dhidi ya makundi ya Kiislam yanayohatarisha usalama nchini Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.