Pata taarifa kuu
TANZANIA-UJERUMANI

Waziri mpya wa mambo ya kigeni wa Ujerumani azuru Tanzania

Waziri mpya wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas, amewasili nchini Tanzania na kuzungumza na makamo wa raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani akikaribishwa na makamo wa raisi wa tanzania Samia Suluhu na Waziri wa mambo ya kigeni Balozi Augustine Mahiga
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani akikaribishwa na makamo wa raisi wa tanzania Samia Suluhu na Waziri wa mambo ya kigeni Balozi Augustine Mahiga Twiter/Samia Suluhu
Matangazo ya kibiashara

 

Taarifa ya kuwasili kwake imethibitishwa na makamo wa raisi Samia Suluhu kupitia ukurasa wake wa Twita jana jioni.

Heiko Maas alianzia kuzuru nchini Ethiopia, ikiwa ni ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu kuteuliwa katika nafasi hiyo.

Akiwa jijini Addis Ababa, Waziri huyo alikutana na viongozi wa Umoja wa Afrika kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo msaada wa kifedha kutoka Ujerumani.

Nchini Tanzania anatarajiwa kukutana na viongozi wa nchi hiyo, kuzungumzia uhusiano wa nchi hizo mbili ikiwemo ushirikiano wa kiuchumi,lakini pia atawatembelea wanafunzi wanaojifunza lugha ya kijerumani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.