Pata taarifa kuu
UGANDA

Vituo vya redio 23 Uganda vyafungwa kwa kuhamasisha uchawi

Mamlaka ya mawasiliano nchini Uganda UCC juma hili imesimamisha leseni ya vituo zaidi ya 23 vya Redio kwa madai kuwa vimekuwa vikihamasisha uchawi.

Kipaza sauti ambacho hutumiwa katia redio.
Kipaza sauti ambacho hutumiwa katia redio. Zero Creatives/Getyimages
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa mamlaka ya mawasiliano nchini Uganda, Pamela Ankunda, amesema vituo hivyo vinafungwa kwa kushiriki katika kuhamasisha na kutangaza vitu vinavyohusiana na uchawi, kufadhili na kukiuka sheria za kimtandao.

Vituo hivyo ni pamoja na Metro FM, Nile FM, Kagadi Broadcasting Services, Emambya FM, Village Club FM, Radio Kitara, Packwach FM and Tropical FM.

Vituo vingine ni Apex FM, Bamboo FM, Ssebo FM, Eastern Voice FM, Eye FM, Victoria FM, RFM, Kiira FM, Tiger FM, Greater African Radio, Dana FM, Gold FM, Hits FM and Radio 5.

Kifungu cha 41 (ibara ya 1 a na b)  ya sheria ya mawasiliano ya Unganda ya mwaka 2013, imeipa mamla tume ya mawasiliano kusimamisha au kufuta leseni ya chombo chochote cha habari katika misingi ya kufanya makosa yanayojirudia.

Ankunda ameongeza kuwa vituo hivyo vya Redio vilipewa taarifa kabla ya kufungwa na kwamba vilikuwa vikifanya kazi chini ya viwango vya utangazaji vilivyowekwa na mamlaka ya mawasiliano UCC.

Mamlaka ya mawasiliano imeongeza kuwa vituo hivyo vitafunguliwa pale tu vitakapokiri kuwa havitarudia kurusha vipindi vyenye maudhui yanayokatazwa au kufanya vitendo vingine vyovyote vinavyokiuka sheria za kimtandao.

Msemaji wa UCC amevitaka vyombo vya habari nchini humo kutoa mafunzo kwa watangazaji wao kuhusu vitu vinavyoruhusiwa na vile ambavyo haviruhusiwi ili kuepuka adhabu kama hii siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.