Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Mwanasiasa wa upinzani Miguna Miguna afurushwa Kenya

Serikali ya Kenya imemfurusha mwanasiasa wa muungano wa upinzani, Nasa, Miguna Miguna na kupelekwa nchini Canada, kwa mujibu wa wakili wake Cliff Ombeta.

Kiongozi wa NASA Raila Odinga akiapa Januari 30 2018, kwenye opicha akionekana Miguna Miguna (kushoto).
Kiongozi wa NASA Raila Odinga akiapa Januari 30 2018, kwenye opicha akionekana Miguna Miguna (kushoto). citizentvkenya
Matangazo ya kibiashara

Katika kile kinachoonekana ni Serikali ya Kenya kutaka kuwanyamazisha wapinzani na kuwashughulikia viongozi walioshiriki kwenye sherehe za kuapishwa kwa kinara wa upinzani Raila Odinga juma moja lililopita, Serikali imeamua kumfukuza nchini humo Miguna Miguna aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa rais Uhuru Kenyatta.

Mmoja wa mawakili wa Miguna, Cliff Ombeta, amethibitisha mteja wake kusafirishwa usiku wa kuamkia leo kwenye ndege ya shirika la KLM kuelekea nchini CANADA nchi ambayo pia yeye ni rais, kwa kile ambacho Serikali inasema mteja wao ni hatari kwa usalama wa taifa.

Siku ya Jumanne mkuu wa jeshi la polisi na kaimu mwendesha mashtaka mkuu walishindwa kumpeleka Miguna katika mahakama kuu ya jijini Nairobi kama ilivyoagizwa na jaji hatua ambayo wadadisi wengi wanahofu kuhusu kuvunjika kwa utawala wa sheria na Serikali kutoheshimu mahakama.

Katika hatua nyingine ofisi ya mwendesha mashtaka ilisema imemshtaki Miguna Miguna kwa tuhuma za uhaini huku wakishindwa kumfikisha mahakamani.

Jana Jumanne polisi jijini Nairobi na atika mji wa Kisumu walikabiliana na mamia ya waandamanaji waliokuwa wanashinikiza kuachiwa kwa Miguna huku wakiikashifu Serikali kwa kutaka kurejesha utawala wa mabavu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.