Pata taarifa kuu
UGANDA-TANZANIA-BURUNDI

Rais wa Uganda alaani uamuzi wa ICC kuichunguza Burundi

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amelaani uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa uhalifu wa kivita ICC ambayo imemwagiza mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo kuanzisha uchunguzi dhidi ya mgogoro wa Burundi.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni DR
Matangazo ya kibiashara

Rais Museveni ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema ICC inaingilia mambo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki bila kuwahusisha viongozi wa Jumuiya hiyo jambo ambalo sio sahihi na linarudisha nyuma juhudi za kutafuta amani ya Burundi.

 

Akizungumzia uamuzi huo Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ambaye amehitimisha ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Uganda hapo jana amesema hatua hiyo inarudisha nyuma hatua zilizochukuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo iliunda Kamati ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi inayoongozwa na Mhe. Rais Museveni na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa.

 

Rais Magufuli amesema hali ya Burundi sio mbaya kama inavyotangazwa kwa kuwa tayari wakimbizi wengi waliokuwa Tanzania wamerejea Burundi na wengine wanaendelea kurejea, na pia viongozi wanaosuluhisha mgogoro huo wamepanga kukutana tarehe 23 Novemba, 2017 kwa lengo la kuendeleza mchakato wa kutatua mgogoro huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.