Pata taarifa kuu
BURUNDI-VYOMBO VYA HABARI

Waandishi wa habari wawili wakamatwa mjini Bujumbura

Nchini Burundi, waandishi wa habari wawili walikamatwa Jumapili hii na vikosi vya usalama. Waandishi hao wa habari ni pamoja na Julia Steers kutoka Marekani ambaye anaishi mjini Nairobi. Aliachiliwa baada ya masaa sita akiwa kizuizini.

© RFI-KISWAHILI
Matangazo ya kibiashara

Julia Steers ameelezea wasiwasi wake kuona Gildas na drevea wake wanaendelea kuzuiliwa wakati yeye tayari amaeachiliwa huru.

Hata hivyo, mwandishi wa habari wa Burundi Gildas Yihundimpundu mbaye alikua akishirikiana na Bii Steers, na dereva wake, wanaendelea kusikilizwa na Idara ya ujasusi.

"Ilikua saa 2:00 asubuhi, wakati tulipowasili eneo la Mutakura, kaskazini mwa mji wa Bujumbura ambapo tulikua tulipanga kufanya kazi yetu ya uandishi wa habari, kupiga picha na kadhalika. Baada ya dakika 20 tuliona jeshi la polisi likitusimamisha tulipokua ndani ya gari, na kisha kuzuia barabara. Walikua na hasira, na waliendelea kuuliza kwa lugha ya Kirundi tulichokuwa tukifanya huko."

Walituzuia takribani saa moja, kisha polisi walikuja, maafisa wa Idara ya ujasusi na wajumbe wa Baraza la Kitaifa Linalochunguza kazi ya waandishi wa habari (CNC) ili kuangalia kuwa tunatimiza vibali tulivyokua navyo. Nilikuwa pamoja na Gildas, mwandishi wa habari wa Burundi na ambaye mara nyingi nashirikiana naye kwa kazi hii ya uandishi wa habari na ambaye pia anafanya kazi na BBC. Alikamatwa, na kupelekwa katika ofisi ya Idara ya ujasusi, sawa na dereva wetu anayejulikana kwa jina la Pascal na ambaye hahusiki na jambo hili .

Polisi ilisema kuwa Gildas hajasajiliwa na Baraza la Kitaifa Linalochunguza kazi ya waandishi wa habari (CNC). Lakini hawajatoa sababu za kukamatwa kwake, na wala hawakutaka niwe pamoja naye, amesema Bii Steers. "Walisisitiza kuwa ni mambo yanayowahusu warundi peke yao. Nina wasiwasi sana, nadhani hawana sababu ya kuwazuia watu hawa wawili. "

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, Pierre Nkurikiye, Julia Steers aliachiliwa baada ya kusikilizwa na Baraza la Kitaifa Linalochunguza kazi ya waandishi wa habari (CNC), ambalo lilikiri kwamba alikuwa na vibali halali. Na alikabidhiwa ubalozi wa Marekani mjini Bujumbura.

Hata hivyo, Gildas Yihundimpundu bado yuko chini ya ulinzi katika ofisi ya Idara ya ujasusi (SNR). CNC imethibitisha kwamba hajasajiliwa kama mwandishi wa habari. Pia anahojiwa kuhusu madai ya kupotosha ushahidi. Kwa mujibu wa polisi waandishi hao wa habari walikamatwa wakiwa karibu na karibu la pamoja, ambako inakisiwa kuwa wafuasi wa chama madarakani cha CNDD-FDD waliuawa na kuzikwa hapo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.