Pata taarifa kuu
BURUNDI-EU-KUFUKUZWA

Serikali ya Burundi yawataka Wazungu kuondoka

Jumamosi hii Machi 16, Makamu wa kwanza wa rais wa Burundi, Gaston Sindimwo amewataka raia wa kigeni kutoka katika nchi za Magharibi waishio katika ardhi ya Burundi kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo.

Askari polisi ya Burundi baada ya mfululizo wa mashambulizi ya guruneti katika mji wa Bujumbura, Februari 15, 2016.2016.
Askari polisi ya Burundi baada ya mfululizo wa mashambulizi ya guruneti katika mji wa Bujumbura, Februari 15, 2016.2016. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Bwana Sindimwo ameyasema hayo Jumamosi asubuhi wakati wa maandamano ya amani yanayofanyika kila Jumamosi. Maandamano yalioandaliwa na utawala wa Bujumbura mikoani kote.

Tamko hilo linakuja wakati ambapo viongozi wa Burundi wanazichukulia nchi za Magharibi kuunga mkono, kwa mujibu wa viongozi hao, wanasiasa na wanajeshi waliohusika katika jaribio la mapinduzi. Serikali ya Burundi imekua ikiwachukulia watu wote wanaopinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza au wale wote walioandamana kuwa ni magaidi.

Hivi karibuni Umoja wa Ulaya, Marekani, na Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa walichukua hatua ya kusimamisha misaada yao waliokua wakiitolea Burundi kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea kushuhudiwa nchini humo pamoja na serikali kukataa katu katu mazungumzo na wadau wote ikiwa ni pamoja na upinzani ulio ukimbizini nje ya nchi.

Wakati huo huo Mkuu wa Idara ya ujasusi katika jeshi Luteni Kanali Alexandre Mbazumutima ametoweka tangu Jumamosi Aprili 16. Lakini wengi wanaamini kuwa ametoroka na kukimbilia mafichoni. Mpaka sasa jeshi halijasema lolote kuhusu kutoweka kwa afisaa huyo wa juu katika jeshi. Hata hivyo hali ya kutoaminiana kati ya jeshi imeendelea kushuhudiwa nchini Burundi kati ya wanajeshi wa zamani (EX- FAB) na baadhi ya wapiganaji wa zamani, hasa kutoka katika kundi la zamani la waasi la CNDD-FDD walioingizwa katika jeshi na kuunda jeshi jipya la Ulinzi linalowakilisha makabila yote nchini humo (FDN).

Katika maeneo mbalimbali nchini humo, miili ya watu waliouwawa katika mazingira ya kutatanisha imeendelea kuokotwa. Upinzani na utawala nchini Burundi, kila upande umeendelea kunyooshea kidolea cha lawama upande mwengine.

Katika msitu wa Rukoko, Magharibi mwa mkoa wa Bubanza kilomita 15 na mji wa Bujumbura mapigano yamekua yakiendelea kati ya jeshi na wapiganaji wa kundi la waasi la FNL linaloongozwa na jenerali Aloys Nzabampema mtoro katika jeshi la Ulinzi (FDN).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.