Pata taarifa kuu

Burundi: Mwanahabari azuiliwa na idara ya Upelelezi

Nchini Burundi kuna mwanahabari ambaye anazuiliwa tangu Jumamosi na Idara ya upelelezi ya nchi hiyo (SNR) jijini Bujumbura, familia yake imeliambia shirika la habari la AFP, na hivyo kuzua wasiwasi mkubwa kwa uhuru wa vyombo vya habari katika nchi hii ya Afrika Mashariki.

Sio mara ya kwanza kwa wanahabari nchini Burundi kulengwa au kuzuiliwa. Mnamo mwezi wa Mei 2023, mwanahabari Floriane Irangabiye alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela akishutumiwa "kuhatarisha usalama wa taifa".
Sio mara ya kwanza kwa wanahabari nchini Burundi kulengwa au kuzuiliwa. Mnamo mwezi wa Mei 2023, mwanahabari Floriane Irangabiye alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela akishutumiwa "kuhatarisha usalama wa taifa". AFP - ONESPHORE NIBIGIRA
Matangazo ya kibiashara

Sandra Muhoza, 42, ni mwandishi wa habari wa chombo cha habari cha mtandaoni cha La Nova Burundi, ambacho kinadaiwa kuwa karibu na utawala. Bi. Muhoza aliitika mwaliko wa mtu tajiri na mfuasi mwenye ushawishi katika chama tawala CNDD-FDD siku ya Jumamosi, familia yake imeliambia shirika la habari la AFP

Mumewe ambaye alikuwa hana habari yoyote kutoka kwake, alipokea ujumbe wa simu siku ya Jumapili ukimwambia "mke wako anazuiliwa katika makao makuu ya idara ya upelelezi (SNR)." Ujumbe huo ulimtaka amletee nguo na vifaa vingine ambavyo anahitaji, amesema mmoja wa watu wa familia yake, akisema "ana wasiwasi mkubwa, lakini na matumaini baada ya ujumbe huo kutoka idara ya upelelezi ukimaanisha kwamba bado yuko hai."

Sababu za kukamatwa kwake, hazijafahamishwa kwa familia. "Tuna wasiwasi mkubwa na kukamatwa kwa mwenzetu, kwa sababu kufikia sasa hatujajua sababu za kuzuiliwa kwale, amesema kwa upande wake mkurugenzi wa Gazeti hili la mtandaoni la La Nova Burundi, Pascal Ndayisenga.

Sio mara ya kwanza kwa wanahabari nchini Burundi kulengwa au kuzuiliwa. Mnamo mwezi wa Mei 2023, mwanahabari Floriane Irangabiye alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela akishutumiwa "kuhatarisha usalama wa taifa".

"Wanahabari nchini Burundi wanaishi kwa uoga mkubwa wa kufanyiwa vitisho, kufanyiwa unyanyasaji au kukamatwa, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Wanahabari Wasio na Mipaka (RSF), ambalo liliiweka Burundi mnamo mwaka 2023 kwenye nafasi ya 114 kwa jumla ya nchi 180 katika suala la uhuru wa vyombo vya habari. Siku ya Jumapili, Maaskofu wa Burundi walilaani katika ujumbe uliosomwa katika kanisa zote nchini humo kile walichokiita jaribio la kuingia katika "mfumo wa chama kimoja", mauaji ya kikatili kwa watu wanaoshikiliwa na vyombo vya dola, na kutokujali au kutokuadhibu watu wanaotuhumiwa uhalifu mbalimbali nchini humo.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, aliyemrithi Pierre Nkurunziza, baada ya kifo chake mnamo mwaka 2020, alipewa maua yake na kupongezwa na jumuiya ya kimataifa kwa kuiweka Burundi, hatua kwa hatua, kwenye na fasi nzuri baada ya kutengwa kimataifa kwa miaka mingi.

Lakini hajafanikiwa kukomesha tabia ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Na Burundi, ambayo haina bandari kufikia bahari, ni nchi masikini duniani kwa suala la Pato la nje kwa wakazi wake, kulingana na Benki ya Dunia, ikiwa na 75% ya wakaazi wake Milioni 12 ambao wanaishi chini ya kiwango cha kimataifa cha umasikini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.