Pata taarifa kuu

Tanzania : Mafuriko yamesababisha vifo vya watu 58

Dar es Salaam – Serikali ya Tanzania imesema mvua inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, na kusababisha mafuriko makubwa, imesababisha vifo vya watu 58 na watu zaidi ya laki mbili wanahitaji msaada wa chakula.

Ramani ya nchi ya Tanzania
Ramani ya nchi ya Tanzania © https://wwwnc.cdc.gov/
Matangazo ya kibiashara

Tangu April Mosi mwaka huu mpaka sasa Mvua hizi zimesababisha vifo vya watu hao katika Mikoa ya Arusha, Dar es salaam, Geita, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Rukwa Huku Morogoro na Pwani ikipata athari kubwa zaidi Mbali na vifo.

Hawa hapa ni baadhi ya raia walioathirika.

‘‘Eneo lote ni maji, kuaanzia makaazi ya binadamu hadi kwenye mashamba.’’ ‘‘Kwa kweli tumekufa na tunaendelea kufa.’’ Walisema baadhi ya walioathirika.

00:11

Walioathirika na mafuriko nchini Tanzania

Katika Mikoa hiyo miwili nyumba zaidi Elfu nane zimebomoka na Mashamba Ekari zaidi ya Elfu 76 na hivyo kuathiri kaya zaidi ya Elfu 10, ambazo zinahitaji msaada wa Chakula ili kuzinusuru na Baa la Njaa, Mobhare Matinyi ni Msemaji wa serikali ya Tanzania.

‘‘Jumla ya tani elfu saba mia nne na ishirini za chakula na nafaka zinahitajika kukidhi mahitaji ya waathirika laki moja elfu 36.’’ alisema Mobhare Matinyi ni Msemaji wa serikali ya Tanzania.

00:24

Mobhare Matinyi ni Msemaji wa serikali ya Tanzania

Mbali na Mafuriko katika mikoa hiyo, Mkoani Mbeya Mlima Kawetele katika kata ya Itezi umeporomoka na kuangukia nyumba zaidi ya 30, na bado Mvua hizi zinaendelea kunyesha nchini.

Soma piaTanzania: Mafuriko yashuhudiwa jijini Dar es Salaam

Steven Mumbi/Dar es Salaam/RFi Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.