Pata taarifa kuu

Malalamiko yawasilishwa kuhusu vifo vya wanajeshi wawili wa Ufaransa nchini Rwanda

Mahakama ya Ufaransa imepokea malalamiko yakitaka "ufafanuzi" kuhusu vifo vya wanajeshi wawili wa Ufaransa waliouawa mwanzoni mwa mauaji ya kimbari ya Watutsi nchini Rwanda. Bado mwanga haujatolewa kuhusu mazingira ya kutoweka kwa René Maïer, Alain Didot na mkewe Gilda mwanzoni mwa mwezi Aprili 1994. Malalamiko yaliyowasilishwa na shirika la Survie kutoka Ufaransa na ndugu wawili wa familia ya Gilda Didot wakishutumu makosa ya "uhalifu wa kivita", "kuua bila kukusudia" ” na “kughushi”.

Wanajeshi wa Ufaransa wakipita mbele ya familia ya Wanyarwanda mnamo Juni 26, 1994, huko Kayove.
Wanajeshi wa Ufaransa wakipita mbele ya familia ya Wanyarwanda mnamo Juni 26, 1994, huko Kayove. © Pascal Guyot / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Aprili 8, 1994, Alain Didot na mkewe Gilda Didot waliripotiwa kufariki na mashahidi. Miili yao na ule wa mtunza bustani wao Mnyarwanda ilipatikana katika bustani ya jumba lao siku nne baadaye. Mwili wa René Maïer ulipatikana siku iliyofuata.

Wakili Hector Bernardini anakumbusha kwamba njia nyingi zimeendelea kuchunguzwa katika kesi hii: “Bado kuna mashahidi wanaodaiwa kuwa walishuhudia mauaji hayo. Bado kuna wanajeshi ambao wako tayari kutuambia, ikiwa kweli wahanga walijeruhiwa kwa risasi na sio watu waliokatwa kwa mapanga. Hii itatubainishia kwamba waliuawa na maafisa wa serikali na sio mauaji ya wanamgambo. "

Wanajeshi hao wawili, ambao walikuwa maafisa wataalamu wa mitambo ya radio, waliweza kusikia ujumbe ukifichua mazingira ya shambulio dhidi ya ndege ya rais kutoka kabila la Wahutu Juvénal Habyarimana Aprili 6, 1994.

François Graner, kutoka chama cha Survie, anahoji hasa uhalisi wa vyeti vya vifo. Hizi vilitengenezwa huko Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati kabla ya miili hiyo kurejeshwa nchini Ufaransa.

"Ni vyeti bandia. Tena wako wanane kati yao na maneneo yao yanakinzana, François Graner anasema. Vyeti feki hivi vilitengenezwa kwa kompyuta. Hata hivyo, wakati huo, huko Bangui, kulikuwa na kompyuta moja tu na ilikuwa ya makao makuu ya vikosi vya Ufaransa. Kwa hivyo, ikiwa majaji wanataka kuanza kusikiliza kesi hiyo, jambo la kwanza ambalo wanatakiwa kufanya, watahoji makao makuu vikosi vya Ufaransa wakati huo na wataona ni nani aliyetengeneza vyeti hivi. "

Hakuna uchunguzi wa maiti ulifanywa, na hakuna uchunguzi wowote ambao umefunguliwa kuhusu mauaji haya watu watatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.