Pata taarifa kuu

Rais Ruto na Museveni wamejadili azma ya Odinga kuongoza tume ya AU

Nairobi – Nchini Uganda, rais Yoweri Museveni amekutana na mwenzake wa Kenya William Ruto ambapo wamezungumzia nia ya waziri mkuu wa zamani wa kenya Raila Odinga kutaka kuongoza tume ya Umoja wa Afrika (AU).

Rais wa Kenya William Ruto, mwenzake wa Uganda Yower Museveni, wamejadiliana kuhusu nia ya Odinga kuongoza tume ya AU.
Rais wa Kenya William Ruto, mwenzake wa Uganda Yower Museveni, wamejadiliana kuhusu nia ya Odinga kuongoza tume ya AU. © William Ruto
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa Odinga, anatafuta uungwaji mkono kutoka nchi za Afrika kutimiza ndoto yake ya kumrithi mwenyekiti wa sasa wa AU, Moussa Faki Mahamat ambaye muda wake unatarajiwa kukamilika mwezi Februari mwaka wa 2025.

Rais Museveni alikuwa mwenyeji wa rais Ruto na kinara wa upinzani nchini kenya, Raila Odinga nyumbani kwake katika eneo la Kisozi nchini Uganda.

Odinga kupitia ukurasa wake wa X, zamani ukiitwa Twitter, ameeleza kuridhishwa na hatua ya rais Museveni kuunga mkono azma yake. 

Kikao cha viongozi hao watatu kimeonekana kuwashangaza raia wengi katika nchi zote mbili. Katika kipindi cha miezi michache iliopita, Odinga alionekana kupinga na kuukashifu uongozi wa rais Ruto, Uganda na Kenya nazo zikionekana kuwa na mvutano wa kiplomasia.

Mwaka uliopita, Odinga, aliongoza msururu wa maandamano dhidhi ya serikali ya rais Ruto kutokana na kile upinzani ulidai ni kupanda kwa gharama ya maisha.

Katika ukurasa wake wa X, rais Ruto alieleza kuwa wamekubaliana kuhusu masuala ya yaliokuwa yakiathiri usambazaji wa bidhaa za petroli kati ya mataifa ya Kenya na Uganda na kwamba baadhi ya changamoto zilikuwa zinatatuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.