Kenya: Odinga akanusha ripoti kuwa atamuunga mkono Kalonzo 2027
Nairobi – Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, amekunusha ripoti za vyombo vya habari kwamba atamuunga mkono makomo wa rais wa zamani, Kalonzo Musyoka kuwania urais kwenye Uchaguzi wa mwaka 2027.
Imechapishwa:
Kupitia msemaji wake Raila Odinga, amesema sifa alizompa mwandani wake kisiasa siku ya jumapili hazimaanishi atamuunga mkono kwenye uchaguzi wa mwaka 2027 kama ilivyokuwa imerpotiwa na baadhi vya vyombo vya habari.
Odinga amesema ni mapema sana kutangaza mgombea urais miaka minne kabla ya kufanyika kwa uchaguzi akisema watatangaza mgombea wao mwaka mmoja au miezi kadhaa kabla ya uchaguzi.
Hatua ya Odinga kumumiminia sifa Kalonzo ilitafusiriwa na wengi kwamba huenda mwanasiasa huyo ambaye amewania urais mara kadhaa, atamuunga mkono Kalonzo kwenye uchaguzi ujao, ila pia imebainika kuwa vyama tanzu vya muungano wa upinzani havifurahishwa na kauli ya Odinga kuonesha wazi huenda akamuunga mkono Kalonzo kwenye uchaguzi ujao, hatua inayotishia kusambaratisha upinzani.
Musyoka, ambaye amewahi kuwa Makamu wa rais mara tatu, aliacha azma yake ya kuwania urais na kumuunga mkono Odinga, mara mbili akiwa mgombea mwenza wake.