Pata taarifa kuu

Kenya: Mazungumzo kati ya upinzani na serikali kuendelea

Raundi nyingine ya mazungumzo ya kujaribu kupata muafaka kati ya Serikali ya Kenya na upinzani, inatarajiwa kuendelea tena hivi leo kukiwa na matumaini ya kupatikana makubaliano.

Mazungumzo hayo yanafanyika kutafuta muafaka kati ya serikali na upinzani
Mazungumzo hayo yanafanyika kutafuta muafaka kati ya serikali na upinzani AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Baada ya wiki kadhaa za maandamano ya upinzani, kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha na shinikizo za kuifanyia marekebisho Tume ya Uchaguzi.

Kikao hiki kinaendelea kuratibiwa na rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, yanatarajiwa kutoa suluhu ya mvutano unaoendelea kati ya kinara wa upinzani Raila Odinga na Serikali, ambapo kila upande ulichagua timu ya watu watano.

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo ndiye mratibu wa mazungumzo hayo
Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo ndiye mratibu wa mazungumzo hayo © dailypost

Mazungumzo yanaanza wakati mwishoni mwa juma lililopita Seneta wa Marekani Chris Andrew Coons, ambaye alihusika pakubwa mwaka 2018 kumpatanisha rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, akikutana na rais William Ruto na Odinga.

Dr Brian Mutie, ni mchambuzi wa masuala ya siasa akiwa Kenya.

“Mazungumzo yatazaa matunda iwapo pande zote mbili ziko kwenye hali ya kuweka mambo wazi.” alisema Dr Brian Mutie, ni mchambuzi wa masuala ya siasa akiwa Kenya.

00:36

Dkt Brian Mutie, ni mchambuzi wa masuala ya siasa akiwa Kenya

Muungano wa upinzani Azimio uliongoza maandamano mwezi Machi na Julai dhidi ya utawala wa rais William Ruto kupinga kile walichosema ni kupanda kwa gharama ya maisha na kutaka mageuzi katika tume ya uchaguzi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani waliokuwa wakiandamana awali
Polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani waliokuwa wakiandamana awali REUTERS - MONICAH MWANGI

Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini humo yanasema karibia watu 30 walifariki katika maandamano hayo wakati upinzani ukisema rekodi zake zilionyesha watu 50 waliuawa.

Upinzani ulisimamisha maandamano mwezi Aprili na Mei ili kuruhusu mchakato sawa wa mazungumzo ya pande mbili, lakini maandamano yalianza tena baada ya mazungumzo kuvunjika.

Upinzani unaongozwa na Stephen Kalonzo Musyoka,naibu wa rais wa zamani wa Kenya
Upinzani unaongozwa na Stephen Kalonzo Musyoka,naibu wa rais wa zamani wa Kenya AFP - SIMON MAINA

Mazungumzo haya yanafanyika huku wakenya wakiwa na imani kuwa suluhu itapatikana kumaliza mvutano wa kisiasa unaoendelea.

Ruto na Odinga wamesema hawatafanya mazungumzo yoyote ya kugawana mamlaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.