Pata taarifa kuu

Kenya: Mazungumzo kati ya serikali na upinzani yameanza

Mazungumzo kati ya serikali ya Kenya na upinzani, yameanza kufanyika Jumatano ya wiki hii jijini Nairobi, baada ya wiki kadhaa za maandamano ya upinzani, kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha na shinikizo za kuifanyia marekebisho Tume ya Uchaguzi.

Mazungumzo yanalenga kutafuta suluhu ya changamoto zilizoko kwa sasa
Mazungumzo yanalenga kutafuta suluhu ya changamoto zilizoko kwa sasa Β© Kimani Ichung’wah
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yanayoenda kuratibiwa na rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, yanatarajiwa kutoa suluhu ya mvutano unaoendelea kati ya kinara wa upinzani Raila Odinga na Serikali, ambapo kila upande ulichagua timu ya watu watano.

Naibu wa rais wa zamani Kalonzo Musyoka anaoongoza kikosi cha upinzani kwenye mazungumzo hayo
Naibu wa rais wa zamani Kalonzo Musyoka anaoongoza kikosi cha upinzani kwenye mazungumzo hayo Β© Kimani Ichung’wah

Muungano wa upinzani Azimio uliongoza maandamano mwezi Machi na Julai dhidi ya utawala wa rais William Ruto kupinga kile walichosema ni kupanda kwa gharama ya maisha na kutaka mageuzi katika tume ya uchaguzi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kalonzo Musyoka, makamu wa rais wa zamani wa Kenya, ndie anaongoza ujumbe wa upinzani.

β€œTunashirikiana na kujadiliana kwa nia njema na kwa dhati kutafuta suluhisho linalofaa kwa Wakenya wote, pili tunatafuta suluhisho linaloshugulikia haki na masilahi ya wakenya wote.” alisema Kalonzo Musyoka, makamu wa rais wa zamani wa Kenya.

00:31

Kalonzo Musyoka, mwakilishi wa upinzani kwenye mazungumzo

Kwa upande wa serikali ukiongozwa na Gavana Cecil Mbarire, nao umesema unashiriki mazungumzo hayo kwa nia njema.

β€œTuko hapa kama mrengo wa Kenya kwanza kwa sababu nchi yetu ni muhimu kuliko sisi binafsi na tumetumwa hapa na rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto kuja kuketi na ndugu zetu ilikupata suluhu ya mambo yanayoletwa mezani.” alieleza Gavana Cecil Mbarire.

00:41

Gavana Cecil Mbarire, Mwakilishi wa serikali kwenye mazungumzo

Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini humo yanasema karibia watu 30 walifariki katika maandamano hayo wakati upinzani ukisema rekodi zake zilionyesha watu 50 waliuawa.

Upinzani ulisimamisha maandamano mwezi Aprili na Mei ili kuruhusu mchakato sawa wa mazungumzo ya pande mbili, lakini maandamano yalianza tena baada ya mazungumzo kuvunjika.

Kiongozi wa wengi kwenye bunge la kitaifa nchini humo Kimani Ichungwa anawakilisha upande wa serikali kwenye mazungumzo hayo
Kiongozi wa wengi kwenye bunge la kitaifa nchini humo Kimani Ichungwa anawakilisha upande wa serikali kwenye mazungumzo hayo Β© Kimani Ichung’wah

Mazungumzo haya yanafanyika huku wakenya wakiwa na imani kuwa suluhu itapatikana kumaliza mvutano wa kisiasa unaoendelea.

Ruto na Odinga wamesema hawatafanya mazungumzo yoyote ya kugawana mamlaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.