Pata taarifa kuu

Kenya : Mazungumzo kati ya upinzani na serikali yanatarajiwa kuaanza

Nairobi – Nchini Kenya, muungano wa upinzani Azimio la Umoja, One Kenya, umetangaza orodha ya wajumbe wake watano, wanaotarajiwa kukutana na wale na serikali, kushiriki kwenye mazungumzo ya kisiasa, chini ya rais wa zamani wa Nigeria, Olesugun Obasanjo.

Mazungumzo kati ya upande wa serikali na upinzani yanatarajiwa kuaanza kumaliza mvutano yao
Mazungumzo kati ya upande wa serikali na upinzani yanatarajiwa kuaanza kumaliza mvutano yao AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Upande wa upinzani utaongozwa na aliyewahi kuwa Makamu wa rais Kalonzo Musyoka. Upande wa serikali haujataja ujumbe wake, ili kuunda kamati hiyo ya wajumbe 10.

Kikosi cha upande wa serikali kitajiunga na kile kilichochaguliwa na mrengo wa upinzani uoongozwa na Raila Odinga kwa mazungumzo ya pande mbili.

Raila Odinga na mrengo wake wamekuwa wakishinikiza kupunguzwa kwa gharama ya maisha
Raila Odinga na mrengo wake wamekuwa wakishinikiza kupunguzwa kwa gharama ya maisha AP - Khalil Senosi

Hata hivyo, kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo, pande hizo mbili zinatofautiana masuala ya kuzungumzia huku kila upande ukivuta upande wake. Mark Bichachi ni mchambuzi wa masuala ya siasa nchini humo.

“Ukitazama namna ambavyo wanasiasa wanavyoongea kusema kwamba mazungumzo yamekaribishwa yataenda mbali kujenga Kenya, utaona kwamba wanasiasa wengi wanaongea ni kama vile mazungumzo tayari yashakubalika na wanasiasa wakuu nchini humo.’’ alisema Mark Bichachi ni mchambuzi wa masuala ya siasa akiwa nchini kenya.

00:39

Mark Bichachi ni mchambuzi wa masuala ya siasa

Upinzani umeorodhesha gharama ya maisha, ukaguzi wa matokeo ya kura ya mwaka 2022, kuundwa upya kwa tume ya uchaguzi  IEBC, ushirikishwaji katika masuala ya kitaifa na heshima kwa vyama vya kisiasa kwa mujibu wa Katiba.

Hata hivyo, rais alishikilia kuwa kupunguzwa kwa gharama ya maisha kamwe hakutakuwa sehemu ya mazungumzo hayo kwani ni jukumu la serikali.

Raia wa Kenya wamekuwa wakitoa kwa serikali ya Ruto kushugulikia suala la kupanda kwa gharama ya maisha
Raia wa Kenya wamekuwa wakitoa kwa serikali ya Ruto kushugulikia suala la kupanda kwa gharama ya maisha REUTERS - MONICAH MWANGI

Timu hiyo ya watu 10 itajumuisha wajumbe wanne kutoka nje ya bunge, wawili kutoka kila upande, viongozi wa bunge la Kitaifa walio wengi na walio wachache, na wabunge wanne wa ziada - wawili kutoka kila upande.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.