Pata taarifa kuu

Tanzania: Godbless Lema amerejea nyumbani

NAIROBI – Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania, Godbless Lema, ambaye amekuwa akiishi uhamishoni nchini Canada tangu mwaka 2020, amerejea nyumbani hapo jana na kulakiwa na wafuasi wa chama chake cha CHADEMA jijini Arusha. 

God Bless Lema mwanasiasa wa Tanzania
God Bless Lema mwanasiasa wa Tanzania © God Bless Lema
Matangazo ya kibiashara

Lema, amesema amerejea Tanzania, kuendeleza harakati za kisiasa. 

“Nimerudi kwa sababu ya wito wa kupigania nchi, ningeweza kusema nisirudi maana kule ni kuzuri hakuna vumbi kuliko hapa mara elfu moja lakini nilisema ntarudi.”amesemaGodbless Lema

Anakuwa mwanasiasa wa pili kurejea nyumbani baada ya Tundu Lissu naye kufanya hivyo, hatua iliyokuja baada ya rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan kuondoa marufuku ya mikutano ya kisiasa kwa vyama vya upinzani. 

Tangu kuondolewa kwa marafuku ya mikutano ya vyama vya kisiasa vya upinzani nchini, vyama hivyo vimeonekana kuendelea na mikutano yake ya kisiasa katika maeneo tofauti ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.