Pata taarifa kuu
AMANI-MARIDHIANO

Sudan Kusini: Karibu waumini elfu moja wakusanyika kumsikiliza Papa Francis

Kiongozi wa kanisa Katolika duniani, Papa Francis, ambaye aliwasili Ijumaa, Februari 3, mjini Juba, Papa Francis anaendelea na ziara yake nchini Sudan Kusini. Yuko katika mji mkuu wa nchi changa zaidi duniani hadi Jumapili kwa "hija ya kiekumene kwa ajili ya amani". Baada ya mikutano yake na viongozi wa nchi siku ya Ijumaa, amehutubia Jumamosi asubuhi Februari 4, kwa makasisi. Takriban waumini elfu moja wamekusanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Thérèse kumsikiliza Papa Francis.

Papa Francis (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waumini wa kanisa kuu la Mtakatifu Theresa mjini Juba, Sudan Kusini, Februari 4, 2023.
Papa Francis (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waumini wa kanisa kuu la Mtakatifu Theresa mjini Juba, Sudan Kusini, Februari 4, 2023. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Wanadini kutoka  dayosisi ya Sudan Kusini lakini pia kutoka Sudan, walisubiri kwa subira ujio wa Papa Francis kwa sauti ya nyimbo za kwaya ya Kanisa hilo.

Sista Mary George anatoka dayosisi ya Malakal, kaskazini-mashariki mwa nchi, na anafanya kazi na wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Sudan: "Kwa hakika ni Kanisa linalofanya kazi kwa ajili ya umoja na amani, ambalo linajaribu kuwapa watu matumaini. Mimi ninayefanya kazi na wakimbizi, matumaini yetu ni kwamba ujio wa papa utatuunganisha na kuleta amani, utulivu katika nchi yetu, kuwezesha wakimbizi kurejea nyumbani, badala ya kukaa katika kambi waliko, kwa miaka kumi. »

Maelewano

Katika hotuba yake, papa ametoa ushauri kwa wanadini kuhimiza maelewano, ndani ya jamii lakini pia ndani ya Kanisa.

"Hatupaswi kamwe kuhudumu kwa kutafuta heshima ya kidini na kijamii, lakini kwa kutembea katikati na pamoja, kujifunza kusikiliza na kuongea," Papa Francis amesema.

"Ujumbe ambao Papa alituelekeza leo, sisi mapadre na maaskofu, wote wa dini na Wakristo, ni kwenda nyumba kwa nyumba kuhubiri amani na uinjilishaji", anasema kwa upande wake Padre Victor Roba Bartolomew ambaye anahudumu katika parokia hiyo ya Sainte Thérèse.

'Kuunganisha watu'

Mseminari Peter Gatkuoth Nhial pia amehudhuria hotuba hiyo: “Kwa kweli Kanisa limepigania amani nchini Sudan Kusini, ili kuwaunganisha watu, ili wasipoteze matumaini na kusali pamoja. Ijapokuwa kuna matatizo katika taifa letu, watu wanatakiwa kujumuika pamoja na kuelewa kwamba sisi sote ni watoto wa baba mmoja. "

Maandamano ya umoja, Papa Francis amejumuika Jumamosi hii jioni na viongozi wengine wawili wa kanisa wanaomsindikiza katika hija hii ya amani nchini Sudan Kusini. Pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbury na Msimamizi wa Kanisa la Scotland, sala ya kiekumene imefanyika kwenye kaburi la John Garang.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.