Pata taarifa kuu

Raila Odinga awasilisha kesi ya kupinga uchaguzi wa Ruto Jumatatu hii

Nchini Kenya macho yote sasa yanaelekezwa katika mahakama ya Juu zaidi baada ya Odinga kukataa matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyompa ushindi makamo rais na rais mteule William Ruto.

Mwanasiasa mkongwe wa Kenya Raila Odinga.
Mwanasiasa mkongwe wa Kenya Raila Odinga. AFP - TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Odinga amepinga matokeo ya urais na ana hadi leo saa nane kuwasilisha ombi lake. Mkenya mwingine yeyote ambaye hakuridhika na matokeo ya uchaguzi anaweza pia kuwasilisha ombi hilo.

Jopo la  majaji saba katika katika Mahakama ya Juu zaidi linatarajia kusikiliza rufaa ya kupinga matokeo iliyowasilishwa na mgombea wa Chama cha Azimio la Umoja-One Kenya.

Majaji hao ni Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Mohamed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaac Lenaola na William Ouko, kulingana na tovuti ya BBC Swahili.

Majaji watatu kati ya saba walibatilisha uchaguzi wa Rais Uhuru Kenyatta mwaka wa 2017. Jaji Mkuu Koome na Jaji Ouko, walijiunga na Mahakama ya Juu Zaidi katikati ya  mwaka wa 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.