Pata taarifa kuu

Ruto kuanza mchakato wa kuunda serikali, Odinga aendelea kupinga ushindi wa mpinzani wake

Nchini Kenya, rais mteule William Ruto amesema muungano wake wa kisiasa wa Kenya Kwanza, utaendelea na mipango ya kuunda serikali, licha ya mpinzani wake Mkuu aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, hapo jana, kukataa kutalbua ushindi wake, na kusema ana mipango ya kutumia kila zote za kikatiba kubadilisha ushindi wa Ruto. 

Rais Mteule wa Kenya William Ruto akihutubia vyombo vya habari katika makazi yake ya makamu wa rais katika Wilaya ya Karen jijini Nairobi, Kenya, Jumatano, Agosti 17, 2022.
Rais Mteule wa Kenya William Ruto akihutubia vyombo vya habari katika makazi yake ya makamu wa rais katika Wilaya ya Karen jijini Nairobi, Kenya, Jumatano, Agosti 17, 2022. AP - Mosa'ab Elshamy
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na viongozi wa muungano wake waliochaguliwa hivi leo, Ruto ameahidi kuwa hakuna sehemu yoyote ya Kenya itaachwa kwenye serikali yake. 

Wakati huo huo muungano wa Azimio la Umoja One Kenya wake Raila Odinga, nao umesisitiza kuwa mgombea wake wa urais alishinda uchaguzi wa wiki iliyopita, na michakato inaendelea kuupinga ushindi wa Ruto? 

Martha Karua, mgombea mwenza wa Odinga amesema, ushindi ni wao, japo umecheleweshwa, utakuja. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.