Pata taarifa kuu

Kambi pinzani katika uchaguzi wa urais Kenya ziko tayari kuzingatia kutunza amani

Nchini Kenya, Seneta wa Marekani Chris Coons amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa kisiasa nchini humo, rais mteule Wiliam Ruto, rais Uhuru Kenyatta na mwanasiasa mkongwe Raila Odinga, baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wiki iliyopita. 

Wakati nchi ikiwa bado imevurugwa kuhusu uhalali wa matokeo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati, muungano wa Azimio la Umoja wa Raila Odinga na muungano wa kisiasa wa William Ruto wa Kenya Kwanza walumbana kuhusu wingi viti katika Bunge la kitaifa.
Wakati nchi ikiwa bado imevurugwa kuhusu uhalali wa matokeo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati, muungano wa Azimio la Umoja wa Raila Odinga na muungano wa kisiasa wa William Ruto wa Kenya Kwanza walumbana kuhusu wingi viti katika Bunge la kitaifa. AFP - TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Seneta Coons, alikutana na rais mteule Ruto  kwanza na kujadiliana kuhusu ushirikiano wa amani, usalama na masuala ya kiuchumi kati ya Kenya na Marekani pamoja na masuala yaliyojikita baada ya uchaguzi. 

Marekani ambayo wiki hii iliwapongeza Wakenya kwa kupiga kura ya amani, imetaka changamoto zozote zilizotokea, zitatuliwe kwa mujibu wa katiba. 

Aidha, amekutana na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga ambaye amepinga ushindi wa Ruto na kumhakikishia kuwa, atatumia njia za kikatiba kupinga matokeo yaliyompa ushindi Ruto. 

Mwanasiasa huyo wa Marekani pia amekutana na rais anayeondoka madarakani Uhuru Kenyatta, ambaye kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu, naye pia ametoa wito wa utulivu katika kipindi hiki. 

Ripoti zinasema kuwa, Seneta Chris Coons alikuwa katika mstari wa mbele kufanikisha maridhiano ya kisiasa kati ya Kenyatta na Odinga mwaka 2018. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.