Pata taarifa kuu

Uchaguzi nchini Kenya: Waangalizi wa kimataifa waridhishwa na zoezi la upigaji kura

Waangalizi wa kimataifa katika ripoti yao ya awali wanasema uchaguzi nchini Kenya uliofanyika siku ya Jumanne, ulikuwa wa utulivu na wapiga kura walipata fursa ya kuwachagua viongozi wanaowapenda licha ya changamoto zilizojitokeza katika baadhi ya vituo kwa wapiga kura kushindwa kutambuliwa na mashine za kieletroniki.

waangalizi kutoka Umoja wa Afrika na Jumuiya ya soko la pamoja la nchi za mashariki na kusini mwa Afrika COMESA, wakiongozwa na rais wa zamani wa Sierra Leon Ernest Bai Koroma pamoja na kusifia namna zoez la kupigia kura lilivyokuwa, katika ripoti yake, wamesema baadhi ya wanasiasa walitumia rasilimali za umma kufanya kampeni.
waangalizi kutoka Umoja wa Afrika na Jumuiya ya soko la pamoja la nchi za mashariki na kusini mwa Afrika COMESA, wakiongozwa na rais wa zamani wa Sierra Leon Ernest Bai Koroma pamoja na kusifia namna zoez la kupigia kura lilivyokuwa, katika ripoti yake, wamesema baadhi ya wanasiasa walitumia rasilimali za umma kufanya kampeni. REUTERS - THOMAS MUKOYA
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa waangalizi kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, rais wa zamani wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika ripoti ya awali ya waangalizi hao, amesema wameridhishwa na zoezi la upigaji kura, na sasa wanatumai matokeo yatadhirisha uamuzi wa Wakenya.

"Waangalizi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, wameridhishwa na namna uchaguzi ulivyofanyika siku ya kupiga kura, wananchi wa Kenya walipewa nafasi ya kuwachagua viongozi wanaowapenda wao kwa uhuru na sasa tunatumai kuwa, zoezi linalosalia, litaheshimu maamuzi ya wapiga kura, kuhusu uchaguzi huu wa mwaka wa 2022," amedokeza jijini Nairobi.

Licha ya changamoto ya idadi ya wapiga kura kutokuwa wengi hasa vijana kutojitokeza, na vifaa vya kieletroniki kutofanya kazi katika baadhi ya matokeo, waangalizi hao wamesifia pia weledi wa maafisa wa Tume ya Uchaguzi kuhusu namna walivyosimamia zoezi la upiga kura.

Hata hivyo, waangalizi kutoka Umoja wa Afrika na Jumuiya ya soko la pamoja la nchi za mashariki na kusini mwa Afrika COMESA, wakiongozwa na rais wa zamani wa Sierra Leon Ernest Bai Koroma pamoja na kusifia namna zoezi la kupigia kura lilivyokuwa, katika ripoti yake, wamesema baadhi ya wanasiasa walitumia rasilimali za umma kufanya kampeni.

"Licha ya kampeni kuwa ya amani  na utulivu na kuangazia maswala yanayowakumba wananchi, kulikuwa na habari za kupotosha na zisizo za kweli. Lakini pia mali ya umma ilitumiwa vibaya, huku makundi ya kuwatisha wapinzani yakitumiwa pia," ameelezea

Thathmini hiyo pia imetolewa na waangalizi wa Kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya, wakiongozwa na Ivan Stefanec, ambaye pia amesema wamekuwa wakifuatialia  namna vyombo vya Habari vinavyojumuisha na kutangaza matokeo ya wanaogombea urais.

"Kuhusu kituo cha kujumuisha matokeo, waangalizi wetu wanafuatilia kwa karibu na pia kile kinachoadikwa kwenye mitandao ya kijamii," amesema.

Waangalizi hawa hata hivyo, wamejiuzuia kusema iwapo uchaguzi nchini Kenya umekuwa huru na haki kwa sababu matokeo ya urais hajatanagzwa rasmi, lakini pia wametoa wito kwa wale ambao hawaridhishwa na matokeo, kuwasilisha kesi Mahakamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.