Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Kenya: Uhuru Kenyatta ahalalisha uungaji wake mkono kwa Raila Odinga

Rais Uhuru Kenyatta amerasimisha uungaji wake mkono kwa aliyekuwa mpinzani wake Raila Odinga katika uchaguzi wa urais utakaofanyika Agosti 9, ambapo hawezi kugombea tena. Hili si jambo la kustaajabisha, lakini bado linasalia kuwa kikwazo kwa makamu wake wa rais William Ruto, ambaye pia ni mgombea urais na ambaye uhusiano naye umeendelea kuzorota.

Rais Uhuru Kenyatta (picha yetu) amerasimisha uungaji wake mkono kwa aliyekuwa mpinzani wake Raila Odinga kuwania katika uchaguzi wa urais.
Rais Uhuru Kenyatta (picha yetu) amerasimisha uungaji wake mkono kwa aliyekuwa mpinzani wake Raila Odinga kuwania katika uchaguzi wa urais. REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Ni wakati wa mkutano mbele ya viongozi wa kambi yake ambapo Rais Kenyatta alitamka wazi kumuunga mkono mpinzani wake wa zamani. Amemwakilisha Raila Odinga kuwa ndiye mwenye uwezo bora wa kutetea maslahi ya nchi na hivyo basi kuwataka wafuasi wake kuunga mkono azma ya yule ambaye, ana na umri wa miaka 76, na anawania kwa mara ya tano.

Usaidizi kamili kwa muda mrefu

Usaidizi huu ulikuwa wazi kwa miezi mingi. Katibu Mkuu wa chama cha Uhuru Kenyatta na viongozi kadhaa wa serikali walikuwa mstari wa mbele wakati Raila Odinga alipojitangaza kuwa mgombea mwezi Desemba mwaka jana. Uhusiano kati ya wawili hao ulianza wakati walipopeana mikono mwaka wa 2018, kitendo ambacho kiliashiria mwisho wa mzozo wa baada ya uchaguzi ambapo walikuwa wamekabiliana vikali.

Hajakomaa kisiasa

Hata hivyo, Uhuru Kenyatta hakukosa kumpigia debe makamu wake wa rais, William Ruto, ambaye pia ni mgombea urais, akimtambulisha kuwa hajakomaa kisiasa kuongoza nchi. William Ruto alijibu. Anasema anaheshimu "maoni" ya rais na haki yake ya kidemokrasia ya kuonyesha upendeleo wake kwa njia hii, lakini anakumbusha kuwa ni Wakenya wanaochagua na kupunguza wigo wa uungwaji mkono huu, "Adui wangu sio kiongozi wa serikali," amesema, lakini Raila Odinga, ninamwomba "asijifiche nyuma ya Uhuru Kenyatta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.