Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Raila Odinga aidhinishwa kuwania kiti cha urais katika uchaguzi ujao

Nchini Kenya, kiongozi wa  muda mrefu wa upinzani na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, ametangaza kuwa atawania tena urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 baada ya kuidhinishwa na vuguvugu la Azimio la Umoja, wakati wa kongamano la kitaifa lililofanyika jijini Nairobi hivi leo. 

Raila Odinga, alipigwa picha wakati wa mahojiano na shirika la habari la  AFP mwezi Septemba.
Raila Odinga, alipigwa picha wakati wa mahojiano na shirika la habari la AFP mwezi Septemba. Simon MAINA AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii itakuwa mara ya tano kwa Odinga mweye umri wa miaka 76, kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha kutaka kuwa rais wa Kenya, baada ya kuidhinishwa na vuguvugu hilo ambalo amekuwa akisema, linalenga kuwaleta Wakenya pamoja. 

Mara ya kwanza, Odinga  aliwania urais  1997, 2007, 2013 na 2017.  

Kiongozi huyo wa muda mrefu wa upinzani amesema, amekubali ombi la azimio la Umoja kuwania urais, huku akiwasilisha mambo 10 ambayo anasema iwapo atashika madaraka atatekeleza, miongoni mwayo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa família masikini zinalipwa Dola zaidi ya Hamsini kila mwezi. 

Wachambuzi wa siasa nchini Kenya, wanasema kuwepo kwa baadhi ya mawaziri katika kongamano hilo, ni dalili kuwa anaungwa mkono na rais Uhuru Kenyatta, ambaye hata hivyo hajasema hilo hadharani. 

Baada ya tangazo hilo la Odinga, uwanja wa kampeni wa kusaka urais umefunguliwa rasmi, na mpinzani wake anatarajiwa kuwa Naibu rais William Ruto, ambaye pia ameendelea kuzunguka nchi nzima akiomba kura, akiahidi kuimarisha uchumi wa Wakenya wa chini. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.