Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Wanasiasa waendelea kunadi sera zao kuelekea Uchaguzi Mkuu

Nchini Kenya, joto la kisiasa kuelekea uchaguzi Mkuu utakaofanyika Agosti 9, linaendelea kupambana moto, huku wagombe wakuu wa nyadhifa ya urais aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga na naibu rais William Ruto wakiendelea kuzunguka nchi nzima wakiomba kura.

Raila Odinga wakati akitangaza rasmi nia yake ya kuwania kwenye kiti cha urais,  Kenya,  Desemba 10, 2021 jijini Nairobi.
Raila Odinga wakati akitangaza rasmi nia yake ya kuwania kwenye kiti cha urais, Kenya, Desemba 10, 2021 jijini Nairobi. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Odinga ambaye ameunda vuguvugu jipya la kisiasa linalofahamika kama Azimio la Umoja na kupata uungwaji mkono na rais Uhuru Kenyatta, siku ya Jumamosi amekuwa  mjini Thika eneo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likimpinga lakini wakati huu mambo yanaonekana tofauti.

Naye Ruto, ameendelea kuahidi kubadilisha uchumi wa wananchi wa chini iwapo ataingia madarakani.

Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Ruto ambaye ametofautiana kisiasa na rais Kenyatta na kuunda chama kipya kutafuta urais, huku Odinga mwanasiasa mkongwe wa upinzani, akiwania sasa kwa mara ya tano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.