Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA

Mbowe akabiliwa na mashitaka ya ugaidi ikiwemo mauaji ya viongozi wa serikali

Nchini Tanzania, kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani cha CHADEMA Freeman Mbowe amepatikana Jijini Dar es salaam baada ya kukamatwa na Jeshi la Polis Jijini Mwanza alipokuwa akiandaa kongamano la kushinikiza mabadiliko ya katiba mpya nchini humo

Freeman Mbowe (hapa ilikuwa Machi 2020) ni mmoja wa anakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya viongozi.
Freeman Mbowe (hapa ilikuwa Machi 2020) ni mmoja wa anakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya viongozi. REUTERS/Emmanuel Herman
Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza nchini Tanzania Ramadhan Ngha'nzi, amethibitisha kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho John Pambalu, tukio lililotokea usiku wa kuamkia June 21 Mwaka huu.

Mwanzoni Jeshi la Polisi tulipata taarifa kwamba mkusanyiko ule ungeleta vurugu na uvunjifu wa amani kwa sababu baadhi yao walipanga kufanya vitendo vya kiuhalifu zaidi ya kukusanyika. Kwa hiyo kulikuwa na katazo la maambuzi ya ugonjwa unao endelea sasa hivi wa changamoto ya kupumua au COVID-19, kwa hiyo tulilazimika kuvunja mkutano ule au kuzia mkutano ule usifanyike.

Hata hivyo Kamanda Ngha'nzi amethibitisha kuwa Mbowe amesafirishwa hadi Jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazo mkabili, huku wenzake 15 wakiendelea kushikiliwa na jeshi hilo katika Mkoa wa Mwanza

Freeman Aikael Mbowe alikamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza na wakati tunaendelea kumhoji ile alfajiri wenzetu wa Dar es salaam vilevile walikuwa wana muhitaji kwa makosa mengine, kwa hiyo ile ile  alfajiri saa moja na nusu tulimsafirisha kwenda Dar es Salaam ambako ana makosa mengine ya jinai, na baada ya mahojiano hayo ya makosa ya jinai kule Dar es saalam nimewasiliana na Kamanda wa Kanda Maalum atamrudisha hapa Mwanza kuungana na wenzake katika kesi ambayo inamkabili, kwa hiyo kwa sasa hivi yupo salama katika kituo cha Polisi Dar es Salaam kwa makosa yaliyo kuwa yana mkabili siku za nyuma

.Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania siku ya Alhamisi kimesema kuwa kiongozi wao na wanachama wengine  huenda wakafunguliwa mashitaka ya ugaidi kufuatia uvamizi wa usiku wa manane jambo ambalo limesababisha wasiwasi kwa wafuasi a chama hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.