Pata taarifa kuu

Wakristo duniani washerehekea Sikukuu ya Krismasi

Shamrashamra za Krismasi zinaendelea kote duniani Jumatatu hii, siku ambayo Wakiristo wanasherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Mwokozi wao Yesu Kristo wakati dunia ikielekeza macho yake katika vita vinavyoendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas kutoka Palestina,  katika Ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya Palestina.

Sikukuu ya Krismasi 2020
Sikukuu ya Krismasi 2020 Church of England
Matangazo ya kibiashara

 

Wakristo duniani kote wanamiminika Makanisani hii leo kuadhimisha siku kuu ya Krismasi. Kulingana na imani ya Kikristo, Krismasi ni siku kuu ambayo wanaamini kuwa Yesu Kristo (Isa) alizaliwa bethlehemu nchini israeli.  Wakiristo wanaamini kuwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo kuliwaletea ukombozi.

Tarehe 25 mwezi Desemba kila mwaka, Wakiristo kote duniani hutumia siku hiyo kwenda Makanisani na baadaye kusherehekea pamoja nyumbani na maeneo mengine kwa kula vyakula na kutoa zawadi.

Mjini Bethlehem nchini Israel, mji ambao Wakiristo wanaamini kuwa Yesu alizaliwa, mwaka huu hakukushuhudiwa shamrashamra kama miaka ya nyuma kutoka na vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas, huku wengine wakiendelea kuandamana kwa kutaka ndugu zao wanaoshikilia na kuli hili la wanamgambo wa Hamas waachiliwe mara moja na Israel ikomeshe vita vyake dhidi ya raia wa Palestina.

Tayari Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, alishatowa tamko la kutaka mapigano kati ya Irael na Hamas yasitishwe haraka iwezekanavyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.