Pata taarifa kuu
NIGER

Covid Niger: Visa vya kwanza vya kirusi cha Delta vyagunduliwa

Kesi za kwanza za aina mpya ya kirusi cha Corona cha Delta zimegunduliwa nchini Niger. Kesi sita zilithibitishwa na Waziri wa Afya ya Umma katika kikao cha Baraza la Mawaziri  cha hivi karibuni. Hatua kadhaa zimechukuliwa.

Kesi sita za ina mpya ya kirusi chaCorona cha Delta ziligunduliwa huko Niamey, Niger.
Kesi sita za ina mpya ya kirusi chaCorona cha Delta ziligunduliwa huko Niamey, Niger. © NigerTZai/wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Kesi sita za kwanza za aina mpya ya kirusi cha Corona cha Delta kutoka India ziligunduliwa katikati ya mwezi Agosti nchini Niger na kuthibitishwa na taasisi ya Pasteur huko Dakar, nchini Senegal. Kulingana na muhtasari uliofanywa na Waziri wa Afya ya Umma katika kikao cha Baraza la Mawaziri cha hivi karibuni, aina mpya ya kirusi cha Corona cha Delta kimegunduliwa kwa watu ambao hawajapewa chanjo.

Kesi hizo sita zilizogunduliwa huko Niamey. Ni raia wanne kutoka Niger, ambao wamerejea nchini mwao na ambao wameambukiza wengine wawili. Baada ya kuhudumiwa haraka, walitibiwa na baadaye kupona.

Watu walioambukizwa kirusi cha Delta na kuwekwa karantini

Pia kulingana na Waziri wa Afya ya Umma, Dk Illiassou Mainassara, mpangilio huo pia uliwezesha kuwaweka karantini watu wengine kumi na tatu walioambukizwa kitrusi cha Delta kutoka Niger, ikiwa ni pamoja na wagonjwa wanane huko Niamey na watano huko Agadez, kaskazini mwa nchi.

Zaidi ya dozi milioni moja za chanjo zimepokelewa nchini Niger tangu mwezi Machimwaka huu, lakini kulingana na Waziri wa Afya ya Umma, kampeni za chanjo zinavutia watu wachache sana. Ni 4% tu ya raia wa Niger  kwa jumla ya wakaazi milioni 21 ndio ambao wamepewa chanjo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.