Pata taarifa kuu
Ukraine - mazungumzo

Catherine Ashton akutana na viongozi wanaogomba nchini Ukraine

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni kwenye Umoja wa Ulaya Catherine Ashton anataraji kukutana na rais wa Ukraine Viktor Ianoukovitch baada mchana wa leo wakati huu Marekani ikitowa wito wa mazungumzo ya serikali na upinzani. Mkuu wa sera wa mambo ya nje kwenye Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amekutana jana na viongozi wa upinzani wakiwemo Vitali Klitschko, Arseni Iatseniouk na Oleg Tiagnybok jijini Kiev ambapo mazungumzo yao yamedumu kwa takriban saa mbili.

rais wa Ukraine Viktor Yanukovich alipokutana na  Catherine Ashton, Desemba 29 jijini Kiev
rais wa Ukraine Viktor Yanukovich alipokutana na Catherine Ashton, Desemba 29 jijini Kiev Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hii leo Ashton atakutana na rais Viktor Ianoukovitch, na baadaye atakutana tena na viongozi hao wa upinzani katika juhudi za Umoja wa Ulaya juu ya kutafuta suluhu ya mzozo unaolikumba taifa hilo tangu mwezi Novemba mwaka jana.

Serikali ya Ukraine huenda ukaitisha uchaguzi kabla ya wakati, kama inavyo ombwa na upinzani, lakini watatuzi wa mizozo wanaonakuwa mabadiliko ya kikatiba yanaweza kuleta suluhusu ya haraka.

Wakati huo huo makam wa rais wa Marekani Joe Biden amemtaka rais wa Ukraine kuendelea na mazungumzo na wapinzani wake na kufikia suluhusu ya kuunda serikali ya pamoja.

Bunge la taifa nchini Ukraine ambalo linaundwa kwa kiasi kikubwa na watu wa karibu na rais Ianoukovitch halijapiga hatuwa yoyote katika kufanya marekebisho ya katiba kama inavyoombwa na upinzani ili kumaliza mzozo unaoendelea.

ghasia za maandamani zimelikumba taifa hilo la Ukraine kwa kipindi kadhaa ambapo waandamanaji wanitaka serikali ya nchi hiyo kukubaliana na Umoja wa Ulaya juu ya maswala ya kuboresha uchumi wa taifa hilo, huku serikali ikisaini mikataba na Urusi badala ya Umoja wa Ulaya.

Upinzani ulikuwa umeapa kuendelea na maandamano hadi kuungusha utawala wa rais Viktor Ianoukovitch.

Hivi karibuni serikali ya Urusi ilizituhumu nchi za Umoja wa Ulaya kuendelea kuchochea machafuko nchini Ukraine, tuhuma ambazo hata hivyo zilitupiliwa mbali na nchi hizo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.