Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-URUSI

Mawaziri wa kigeni mataifa yenye nguvu duniani kujadiliana juu ya mpango wa nyuklia wa Iran,Geneva

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry na wengine sita watafanya kwa mara nyingine mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa iran jumamosi hii huko Geneva nchini Uswisi.

mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka Ufaransa Laurent Fabius, Uingereza William Hague , Ujerumani  Guido Westerwelle na Moscow  Sergei Lavrov watajadiliana Geneva sambamba na John Kerry wa Marekani.
mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka Ufaransa Laurent Fabius, Uingereza William Hague , Ujerumani Guido Westerwelle na Moscow Sergei Lavrov watajadiliana Geneva sambamba na John Kerry wa Marekani. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii itakuwa ni kwa mara ya pili ndani ya majuma mawili ambapo kerry na wakuu wengine watajadiliana katika hotel moja mjini geneva baada ya kukwama kwa mazuzngumzo muhimu ya tarehe 10 novemba.

Msemaji wa Marekani Marie Half amebainisha kuwa Kerry ameamua kurejea kwa mara nyingine kwa matumaini ya kufanikiwa kusonga mbele katika mjadala huo na hatimaye kufanikisha makubaliano.

Waziri Kerry atakutana tena nchini Uswisi na mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka Ufaransa Laurent Fabius, Uingereza William Hague , Ujerumani Guido Westerwelle na Moscow Sergei Lavrov.

Mapema alhamisi Mjumbe mkuu wa Iran katika mazungumzo ya Geneva Abbas Araghachi alionya juu ya kutokuaminiana kama moja ya kikwazo cha mazungumzo hayo yahusuyo nyuklia kati ya mataifa makubwa duniani na nchi ya Iran.

Kikwazo cha kutoaminiana kimekuwa kikubwa hasa katika majadiliano ya mwisho na kuona kuwa ikiwa suala la kukosekana kwa kuaminiana haitawezekana kuendelea na mazungumzo yenye tija kama alivyonukuliwa Abbas Araghachi akisema katika televisheni ya taifa hilo.

Hata hivyo Wachambuzi wa siasa wanaonakuwa hakuna matumaini yoyote ya kupatikana muafaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.