Pata taarifa kuu
EU-SYRIA-URUSI-MAREKANI

Umoja wa Ulaya waondoa vikwazo vya silaha dhidi ya upinzani nchini Syria

Umoja wa Ulaya hatimaye umekubaliana na mpango wa kuwaondolea vikwazo vya kupatiwa silaha kwa waasi wa Syria japokuwa hakuna nchi iliyotangaza kuanza kupeleka silaha hivi karibuni kuhofia kuvunjika kwa mazungumzo ya amani yaliyoandaliwa na nchi za Marekani na Urusi.

Wapiganaji waasi wa Syria wakiwa katika moja ya mapambano na silaha duni kukabiliana na wanajeshi wa Serikali
Wapiganaji waasi wa Syria wakiwa katika moja ya mapambano na silaha duni kukabiliana na wanajeshi wa Serikali Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya ulidumu kwa saa kumi na mbili ambapo kulikuwa na mvutano iwapo waruhusu kusambaza silaha kwa waasi au la, wakati huu ile makataa ya awali ikifikia tamati juma hili.

Akitangaza maamuzi yaliyofikiwa na mawaziri hao, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague amesema kuwa, kwa kauli moja wamekubaliana kuwaondolea vikwazo vya kupatiwa silaha waasi wa Syria na kwamba licha ya hivyo bado vita ni ngumu nchini humo.

Iwapo mataifa hayo yasingeweza kufikia uamuzi huo ingekuwa ni hatua moja nyuma kwa Umoja wa Ulaya katika kuhakikisha wanawasaidia waasi kupambana na serikali ya rais Bashar al-Assad.

Licha ya kupitishwa kwa azimio la kuwaondolea vikwazo waasi wa Syria, bado kuna mgawanyiko miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya huku baadhi yao wakiona kuwa hatua hiyo itachochea kuibuka kwa makundi zaidi ya kigaidi nchini Syria na kutishia usalama wa nchi jirani.

Nchi ambazo waziwazi zilipinga mpango wa kusambaza silaha zaidi kwa waasi ni pamoja na Jamhuri ya Cheki, Austria, Sweeden na Finland.

Katika hatua nyingine Seneta wa Marekani, John McCain amefanya ziara ya ghafla nchini Syria na kukutana na kamanda wa vikosi vya waasi nchini Syria ambapo ameeleza mkakati wake wa kuunga mkono upelekwaji wa silaha kwa waasi.

Hatua hii ya Umoja wa Ulaya inafikiwa wakati huu ambapo nchi za Marekani na Urusi zimeandaa mkutano wa kimataifa mjini Geneva Uswis ambapo zitawakutanisha upande wa waasi na ule wa serikali ya rais Assad ambao ulikubali kwa mara ya kwanza kuhudhuria mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.