Pata taarifa kuu
MAREKANI

Waziri Hillary Clinton aruhusiwa kutoka Hospital baada ya kupatiwa matibabu kwa siku tatu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton ameruhusiwa kutoka Hospital ambako alikuwa anapatiwa matibabu Jijini New York kwa siku tatu akisumbuliwa na tatizo la kuganda damu kichwani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton akitoka Hospital huko New York baada ya kupatiwa matibabu ya siku tatu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton akitoka Hospital huko New York baada ya kupatiwa matibabu ya siku tatu REUTERS/Joshua Lott
Matangazo ya kibiashara

Naibu Msaidizi wa Waziri huyo Philippe Reines ndiye ambaye amethibitisha kutolewa Hospital kwa Clinton jioni ya jana kutokana na hali yake kiafya kutengemaa na hivyo yupo tayari kuendelea na shughuli zake.

Clinton ambaye alilazimika kusherehekea sherehe za kuukaribishwa Mwaka Mpya akiwa Hospital anatarajiwa kurejea kazini punde tu pale ambapo Jopo la madaktari litakapojiridhishwa amepona sawa sawa.

Jopo la Madaktari lililokuwa linamhudumia Clinton limewatoa hofu wanafamilia na hata wananchi ya kwamba Kiongozi huyo atapona kabisa katika kipindi kifupi kijacho kutokana na tiba ambayo amepatiwa.

Kwa upande wake Reines amenukuliwa akisema Clinton atarejea kazini kuendelea na majukumu yaka kama ambavyo Madaktari walivyoshauri baada ya kupona anaweza akaendelea na kazi zake za awali pasi na shaka yoyote.

Clintona ameonekana tena kwa mara ya kwanza tangu aliponekana aliporejea nyumbani baada ya kukamilisha ziara yake ya Ulaya tareje saba mwezi Desemba lakini sasa akiwa amevalia mavazi ya kumkinga na baridi pamoja na miwani myeusi.

Miongoni mwa wale ambao wamethibitisha kutolewa Hospitali kwa Clinton ni pamoja na mtoto wake Chelsea Clinton ambaye kwenye mtandao wa tweeter ameandika akimshukuru Mwenyezimungu ya kwamba mama yake ameruhusiwa kutoka Hospital.

Mapema Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Victor Nuland amenukuliwa akisema Clinton alikuwa anaendelea kufanya kazi kwa njia ya simu kipindi chote ambacho alikuwa Hospital kwa matibabu.

Clinton anatarajiwa kujiuzulu wadhifa wake baada ya kuhudumu kwenye nafasi hiyo kwa miaka minne chini ya rais Barack Obama ambapo nafasi yake itachukuliwa na Seneta John Kerry.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.