Pata taarifa kuu
MAREKANI

Serikali ya Marekani yataka maelezo ya kina toka benki ya Standard Chartered kuhusu benki hiyo kufanya biashara na nchi ya Iran

Uongozi wa benki ya Standard Chartered nchini Marekani umekanusha vikali taarifa iliyotolewa na ofisi ya ukaguzi nchini humo kuwa benki hiyo imeficha na kufanya biashara ya siri na nchi ya Iran kwa njia ya kibenki wakati imetangaza vikwazo.

Ofisi za benki ya Standard Chertered mjini Shanghai China
Ofisi za benki ya Standard Chertered mjini Shanghai China Reuters
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu ofisi ya serikali inayosimamia masuala ya fedha nchini humo iliitaja benki ya Standard chartered kufanya biashara na nchi ya Iran yenye kiasi cha dola bilioni 250 na kutishia kuinyang'anya leseni benki hiyo.

Hii leo menejiment ya benki hiyo imetoa taarifa kwa vyombo vya habari na serikali kukanusha kuhusika na kufanya biashara na nchi ya Iran kwakuwa vikwazo vilivyotangazwana nchi ya Marekani inahusu huduma zote za kibenki.

Biashara hiyo inadaiwa kufanywa kati ya mwaka 2001 hadi 2010 kwa njia ya usiri mkubwa na ofisi ya DFS kuhoji uhalali wa benki hiyo kuendelea kufanya biashara ya fedha na nchi ya Iran kwa njia ya siri.

Serikali ya Marekani imetoa hadi tarehe 15 ya mwezi huu kwa benki hiyo kutoa maelezo ya kina kuhusiana na tuhuma hizo ama sivyo itafutiwa leseni yake ya kufanya biashara nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.